AWESO AAGIZA WABADHIRIFU MRADI WA MAJI KUWEKWA MAHABUSU


Na Lucas Myovela, Arusha.

NAIBU Waziri wa Maji, Juma Aweso (mb),ameamuru jeshi la Polisi wilaya ya Arumeru kuwakamata watumishi watatu , wasimamizi wa mradi wa maji wa Makilenga uliopo katika tarafa ya King'ori wilayani Arumeru Mkoani Arusha kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi huo.


Awali akielekea katika chanzo cha mradi huo Aweso alisimamishwa  njiani na wananchi wa kijiji cha Oldenyong'ilo kilichopo kata ya King'ori Halmashauri ya meru ili waweze kueleza kero zao za maji hasa katika mradi huo mkubwa wa maji uliojengwa kuhudumia tarafa hiyo yenye vijiji 22 katika kata tano.


Mmoja wa wananchi hao aliyefahamika kwa jina la Mwaija Omary,alieleza kuwa kero ya maji katika kata hiyo imekuwa sugu hasa kwa viongozi wasimamizi wa mradi huo  kuweka matabaka ya ugawaji maji kwa kupendelea maeneo yao na kuwafungulia maji wananchi wengine pindi wanapo sikia kuna viongozi wa serikali wanatembelea maeneo hayo.

"Sisi kama wananchi tunaimani sana na mkuu wetu wa wilaya Jerry Muro ila watumishi na wasimazi wakuu wa huu mradi wanatunyanyasa kama sisi siyo binadamu jana usiku wamesika waziri anakuja ndiyo wametufungulia maji na siyo megi tumepata dumu mbili mbili tu na maji tayari yamefungwa tunaomba mtuondolee watu hawa maana watachonganisha wananchi na serikali yao." walisema wananchi hao.

Mara baada ya Aweso kumaliza kutembelea vyanzo vya maji hasa mradi huo wa maji wa Makilenga uliyo gharimu fedha za serikali shilingi Bilioni 3.6 uliyo kamilika mwaka 2015 na kukabidhiwa kwa wajumbe wa bodi ya maji ya Makilenga ili kuhudumia wananchi.

Mradi huo wa Makilenga toka kukamilika kwake umeimarisha upatikanaji wa maji katika vijiji 22 katika kata tano ambazo ni Ngarenanyuki,Leguruki,Kingo'ori,Maruango na Malula.Katika kutoa huduma hizo Mradi huo unakusanya shilingi Milioni tano kwa kila mwezi toka kuanzishwa kwakwe Mwaka 2015.

KICHEFUCHEFU CHA HOTUBA YA MAKILENGA KWA NAIBU WAZIRI WA MAJI.

Naibu waziri: Nimesikiliza kwa makini hotuba yenu ila haijakamilika kama nilivyo taka maana haina mapato na matumizi ya kila mwezi wala kila mwaka nani mwasibu wa mradi huu wa Makilenga na Mwenyekiti wake.

Naibu Waziri: Je mwasibu mnakusanya kiasi gani cha fedha kwa mwezi?, na Mmnesha kaa vikao vingapi vya mpango kazi,na wewe unamuda gani kwenye mradi huu kama mwasibu?

Mhasibu: tunakusanya kwa mwezi shilingi Milioni tano Mh Naibu waziri na mpaka sasa hatujawahi kukaa vikao na muda wangu katika mradi huu ni miaka mitano toka kuanzishwa kwake nilikuwa mhasibu mpaka sasa.

Naibu Waziri: Je Mpaka sasa mnakiasi gani cha fedha toka 2015?

Mhasibu: Miloni moja na Laki mbili Mh waziri.Naibu Waziri: OCD chukua hawa watu weka ndani maana haiwezekani toka mwaka 2015 hadi leo hakuna vikao wala mapato na matumizi na ukusanyaji wa milioni 5 kwa mwezi hadi leo wanayo milioni moja na laki mbili pekee? Huu sio mradi wa matumbo ya watu bali ni mradi wa wananchi na hakuna hata shilingi moja itapotea.

Naibu waziri:Nimuombe fudi wa zamani Mzee Lemali aje hapa mbele.

Naibu waziri : Mzee wangu embu tueleze wewe ulivyo ondoka ulicha account inashilingi ngapi za mradi na umeondoka lini.

Mzee Lemali: Mimi mpaka sasa nina miaka 3 toka niondoke katika mradi huu na tuliacha Milioni 32 katika akaunti ya Mradi na mitambo ya nishati ya Sola kwaa ajili ya kuendeshea na kusukuma pampu za maji.

Naibu Waziri: Mnaona sasa licha ya mradi huu wa makilenga kukusanya Shilingi Milioni tano kwa mwezi lakini mpaka sasa fedha iliyopo bank ni Milioni Moja na laki mbili pekee,Je nini maana ya makusanyo na wapi yanakwenda?

Walio kamatwa katika sakata hilo ni Mwenye kiti wa mradi Bw Godhope Charles,mwasibu wa Mradi Bi Waliaranga Kisetu na fundi msaidizi wa mradi Bw Ndekilo Kaaya huku meneja wa mradi Bw Olenest akiponea chupu chupu baada ya kucheka mbele ya mkutano na kushindwa kujibu maswali na kupewa adhabu ya kukaa masaa 12 kukaa rumande katika kituo cha Polisi usa_river.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewataka wananchi kutokubeba maneno ya vijiweni hususani katika suala la maendeleo na badala yake wawe chanzo cha maendeleo kwa kuisaidia serikali kutunza miundombinu mbali mbali kwa ajili ya maendeleo.

Aidha aliagiza kuwa kupitia mradi huu wa Makilenga wenye viti wote wa jiji 22 ambapo mradi huo unatoa huduma ni lazima wawe kwenye bodi ya maji ya Makilenga ili iwe rahisi kwa viongozi hao kuwasilisha na kutatua kero za wananchi wao kuhusu maji na kupanga mgao sawa na sahihi kwa wananchi wote waliyopitiwa na mradi huo.

"Nilijua tunatatizo katika kusimamia pamoja na ukosaji wa mfumo bora wa usimamizi wa usukumaji wa maji lakinmi nilipo itisha kikao nikaambiwa mtaalamu wa mwanzo aliyekuwa anashughulikia maji haya alitishiwa kuchomewa nyumba yake na yeye kuuwawa na ndipo alipo kimbilia mkoani Iringa,”anasema.

Pia anasema” Ila nimemrudisha kwa fedha zangu mwenyewe Mzee Lemali kwa ajili yeye ni mtaalam nani mzoefu wa mradi huu anajua maji yanapatikana vipi na katika hili naapa hakuna jiwe litakalo salia juu ya jiwe muda wenu sasa umekwisha tupo kwaajili ya kuhakikisha wananchi wanapata maisha bora." Anasema Dc Murro.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post