Na Seif Mangwangi, Arusha
ZAIDI ya Wanataaluma wa ufuatiliaji na Tathmini 1500, wanatarajiwa kushiriki kwenye kongamano la Tano linaloanza kesho Jijini Arusha huku Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba akitarajiwa kufungua Kongamano hilo litakalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini hapa, Leo Septemba 21, 2026 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makala, amesema kongamano hilo linalokutanisha washiriki 1,500 kutoka serikalini, taasisi za umma, sekta binafsi na wadau wa maendeleo litafanyika Kwa siku Tano kuanzia Septemba 22 Hadi 26,02026.
Amesema Waziri Mkuu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Septemba 23, ambapo kongamano hilo litajadili uzoefu, ubunifu na mbinu bora za ufuatiliaji na tathmini, pamoja na namna ya kutumia matokeo yake kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
Kwa mujibu wa Makala, kongamano hilo linalenga kuimarisha mifumo ya kufanya maamuzi inayozingatia ushahidi na data sahihi, kuongeza uwajibikaji na kuboresha utendaji wa taasisi.
Amesema ufuatiliaji na tathmini si zoezi la kiufundi pekee, bali ni msingi wa kupanga na kutekeleza mipango yenye tija, kupima matokeo na kufanya marekebisho kwa wakati ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo 2050, Malengo ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063.
Ofisa Mwandamizi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Charlton Meena, amesema kongamano hilo litatoa fursa kwa viongozi wa serikali, washirika wa maendeleo, sekta binafsi na wananchi kujadili maendeleo na musta kabali wa nchi.
Amesema washiriki 1,500 tayari wamethibitisha kushiriki, huku mada mbalimbali zikitaraiiwa kuiadiliwa katika konaamano hilo lenve kauli mbinu " Kuimarisha tathmini Kwa maendeleo endelevu ya watu".


