Wakulima wa ngano Monduli, Karatu waomba mikopo, mbolea ya ruzuku ili kunufaika na zao hilo

  

Na Seif Mangwangi, Arusha

WAKULIMA wa ngano nchini wamehimizwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ili kupata matokeo mazuri ikiwemo mavuno mengi yenye ubora unaokubalika.


Aidha, wakulima wa zao hilo wameishukuru Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko nchini,(CPB) kwa kuwawezesha kupata mavuno mengi msimu uliopita baada ya kuwakopesha mbegu aina ya  Select na kuwaunganisha na taasisi za fedha wakapata mkopo.


Wakizungumza na waandishi wa habari wakulima hao kutoka katika wilaya za  Karatu na Monduli  wameoimba Serikali iwawezeshe kupata mbolea ya ruzuku na mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kunufaika zaidi na kilimo cha zao hilo.


Afisa Kilimo Msaidizi wa kata ya Monduli Juu, Roy Mruma alisema kuwa kwenye msimu uliopita wa kilimo licha ya kukumbwa na changamoto ya mvua kuwa kidogo na  kuchelewa kwambegu huku wakikosa kupandia na kukuzia lakini waliweza kupata mavuno mazuri kutokana na kuwa na mbegu bora.


“Mbegu ya Select ni nzuri kwa sababu kuna wakulima hawakuweka mbolea lakini waliweza kupata mpaka gunia 11 kwa ekari moja hivyo kama wangeweka mbolea wangeweza kupata gunia 17 mpaka 18 kwa ekari moja,” alisema Mruma na kuongeza.


…Tunawashauri wakulima waandae mashamba mapema waandae na pembejeo ili wazitumie kwa wakati kwani hali ya hewa huwa haisubiri,  pindi mazao yanapokuwa shamba wahakikishe mbolea ya kupanda na kukuzia bila kusahau ya viuatilifu.


…Taratibu za mikopo nadhani wameshaanza na bahati nzuri tumeshafanya kikao cha pamoja na watu wa madawa, watu wa mikopo na kampuni ya mbegu ya Seed Co ambaye ndiyo anazailisha mbegu ya S Select, CPB na Kituo Cha Utafiti wa Kilimo nchini,(TARI)  Seliani  ambao walitoa elimu ya kilimo bora,”.


Mruma alisema kuwa kwa wakulima wa Monduli kuanzia mwezi Januari wanatakiwa kuanza kuandaa mashamba ili inapofika mwishoni mwa mwezi wa pili au mwanzoni mwa mwezi wa tatu waanze kupanda kwa sababu huwezi kupanda mapema sana mazao yataharibika endapo mvua zitanyesha kwa kipindi kirefu.


“Miaka ya nyuma wakulima wa Monduli walikuwa wamejikita kwenye kilimo cha shayiri kwa kuwa ngano ya chakula haikuwa na soko ila tokea msimu uliopita wakulima wamerudi kulima ngano ya chakula baada ya serikali kupitia CPB kuamua kufufua zao hili na kuanzisha kilimo cha mkataba,” alisema Mruma.


Kwa upande wake Mkulima kutoka kijiji cha Lendikinyo,  kata ya Sepeku wilayani Monduli, Daniel Ole Laizer alisema kuwa mbegu ya S Select imempa mavuno mengi sana kwani kwenye ekari moja alipanda kilo 65 za mbegu hiyo na alivuna gunia 18 zenye kilo 100 kwa kila moja.


“Tulipata mbegu ikiwa imechelewa,  tuliipata mwezi wa tatu Lakini na changamoto ya tabia nchi nayo ilichangia kwa kuwa mvua ilikuwa chache lakini tumepata mavuno mengi,” alisema Laizer na kuongeza.


…Ngano ya S Select ni nzuri kwa uzalishaji kwanza inatoa matawi mengi katika shamba ambayo niliweka mbolea inatoa matawi 10 mpaka 12 kwa mche mmoja. Nikaona mvuno yamekuwa mazuri sana japo kuwa nimechelewa kidogo lakini mavuno yaliniridhisha kwa sababu nimepata gunia 18 kwa ekari moja.


…Kwenye eneo  nilioweka mbolea nilipata gunia 18 kwa ekari moja  ila kule ambapo sikuweka mbolea nimepata wastani wa gunia 10 kwa ekari moja kama ningeweka mbolea kote ningekuwa na mfanikio makubwa sana,”.


Laizer aliiomba kamapuni  ya Seed Co wanaozalisha na kusambaza  mbegu ya S Select waweke mashamba darasa ya kutosha kwenye maeneo yao ili wakulima wazidi kupata uelewa wa kutosha juu ya njia bora za kilimo cha zao la ngano.


“Serikali itusaidie tupate mikopo yenye riba nafuu, watusaidie kupata mbolea ya ruzuku na ije kwa wakati ikiwezekana wakati mbegu tunapoletewa ili tuwe na uhakika tunapopanda ngano tunaweka mbolea ya kupandia na baadaye tunaweka ya kukuzia,aliomba Laizer.


Kwa upande wake mkulima mzoefu kutoka wilayani  Karatu, Daniel Pareso alisema kuwa siri kubwa ya kupata mavuno mengi na bora ni kwa mkulima kufanya maandalizi ya shamba mapema kama ambavyo yeye  ameanza kwa kulilema kwa jembe na baadaye chizo tayari kwa kupanda ngano mwezi Machi,2022.


“Mwaka huu 2021 nilipanda mbegu ya ngano ya S Select, mimi nimeipenda sana, imenipa manufaa makubwa sana kwa sababu katika gunia 90 nimepata tani 11 ilikuwa na uzito wa juu sana kwa ekari moja nilipata gunia 12,” alisema Paresso.


Alisema miaka ya nyuma alikuwa akitumia mbegu za kubahatisha kutoka kwa watu mbalimbali nahazikuwa na ubora mzuri ambapo walikuwa wakipata magunia matano mpaka saba kwa ekari moja.


Hata hivyo alibainisha sababu za baadhi ya wakulima kushindwa kupata mavuno mengi kuwa ni maandalizi hafifu ya shamba kwa kile alichodai kuwa wanapanda ngano kwenye shamba ambalo ametoa mazao mengine siku chache zilizopita na wakati mwingine lina majani.


“Unakuta shamba lake amevuna maharage hata hajalilima na kulisawazisha vizuri hapohapo anapanda ngano. Hapo hawezi kupata mavuno mengi, ngano inataka maandalizi ya shamba ya kutosha,” alisema Pareso na kuongeza.

…Hapa kwenye shamba langu liliwekwa shamba darasa eneo tuliloweka mbolea kama inavyoelekezwa na wataalam  tulivuna gunia 10 kwa ekari na eneo ambalo hatukuweka mbolea tumepata gunia tatu kwa ekari.

“Mbolea ni ya muhimu sana kwa sababu mashamba yetu ni ya muda mrefu tumeyarithi kutoka kwa mababu zamani mazao yalikuwa yanakubali bila mbolea lakini sasa ardhi imeshatumiaka sana inahitaji kurutubishwa kwa mbolea,”.


Pareso alisema kuwa siku za nyuma waliacha kulima ngano ya chakula baada ya kukosa mbegu bora kwani walikuwa wanauziana mbegu zilezile walizovuna kwenye msimu ulipita hivyo ikawa haina ubora na kusababisha kuwa haina  soko.


Mwaka huu Serikali kupitia CPB ilikuja na mpango wa kufufua zao la ngano ya chakula ambapo iliamua kuagiza mbegu bora ya ngano ya S select kutoka kampuni Seed CO na kuwakopesha wakulima wa ngano.


Wakulima walionufaika na mpango huo wa kilimo cha mkataba  ni kutoka  mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambapo mbali ya kukopeshwa mbegu waliunganishwa na taasisi za fedha wakapata mikopo.


Baada ya ngano hiyo kukomaa ilinunuliwa na CPB kwa  bei ya juu ya shilingi 800 kiwango ambacho ni cha kikubwa  sana ikilinganishwa na bei iliyokuwa ikilipwa na wanunuzi binafsi ya shilingi 500 kwa kilo.




 


  


 


 


 



 

1 Comments

This is received, thanks for your comments, will come back to you

  1. Unatafuta kampuni halisi ya mkopo wa kifedha ili kupata mkopo wa euro 10,000 hadi euro 10,000,000 (kwa mikopo ya biashara au biashara, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya nyumba, mikopo ya gari, mikopo ya uimarishaji wa madeni, mikopo ya mtaji wa mradi, mikopo ya afya nk. ))
    Au ananyimwa mkopo benki au taasisi ya fedha kwa sababu yoyote ile?
    Omba sasa na upate mkopo halisi wa kifedha. Imechakatwa na kuidhinishwa ndani ya siku 3.
    PACIFIC FINANCIAL LOAN FIRM Sisi ni wakopeshaji wa mkopo wa kimataifa ambao hutoa fedha halisi kwa watu binafsi na makampuni kwa riba ya chini ya 2% tukiwa na kitambulisho halali au pasi ya kusafiria ya kimataifa ya nchi yako ili kuthibitishwa. Malipo ya mkopo huanza mwaka 1 (moja) baada ya. mkopo umepokelewa na muda wa marejesho ni miaka 3 hadi 35.

    Kwa jibu la haraka na kushughulikia ombi lako la mpaka ndani ya siku 2 za kazi
    Wasiliana nasi moja kwa moja kupitia barua hii: pacififinancialloanfirm@gmail.com

    Wasiliana nasi kwa maelezo yafuatayo:

    Jina kamili: ____________________________
    Kiasi cha pesa kinachohitajika kama mkopo: _______________
    Muda wa mkopo: ___________________________________
    Madhumuni ya mkopo: ____________________
    Siku ya kuzaliwa: ___________________________________
    Jinsia: ______________________________
    Hali ya Ndoa: ___________________________________
    Anwani ya mawasiliano: ___________________________________
    Mji / Msimbo wa Eneo: ___________________________________
    Nchi: ______________________________
    Kazi: ___________________________________
    Simu ya rununu: __________________________

    Tuma ombi lako la jibu la haraka kwa: pacififinancialloanfirm@gmail.com

    asante

    Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Victoria Johnson

    ReplyDelete
Previous Post Next Post