WAKAZI ARUMERU WACHEKELEA MIRADI YA MAENDELEO

 Na Seif Mangwangi, Arusha

Utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ikiwemo upatikanaji wa umeme vijijini Katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha, kunatajwa kama moja ya mambo yanayochangia ukuaji wa Uchumi kwa mtu mmoja mmoja na  ongezeko la pato la Taifa.

Kwa miongo kadhaa iliyopita upatikanaji wa  umeme  kwa wakazi wa vijijini  ulikuwa ni ndoto ambayo haikuwa rahisi kufikiwa,kwa sasa mambo yamebadilika kupitia Wakala wa Nishati Vijijini  REA ambapo ndoto imegeuka kuwa kweli.

Diwani mteule wa kata ya Laroi na Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Arusha, Wilayani Arumeru, Ojung'u Selekwa, amesema mradi wa REA umesaidia wakazi wa Arumeru kuendeleza biashara zao kufuatia kuwa na umeme wa uhakika.

Amesema vijana wamefungua vijiwe vya kuchomelea na saluni za kiume katika maeneo mbalimbali Wilayani humo huku kina Mama na wenyewe wakijiajiri kwa kuanzisha maduka ya saluni na kuondokana na tatizo la kukosa ajira, tatizo ambalo lilikuwa likiwasumbua vijana wengine nchini.

Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Arusha na diwani mteule Kata ya Laroi Dkt Ojung'u Selekwa

Maboresho Katika sekta ya elimu , afya  na maji ni baadhi ya mambo mengi yaliofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuhakisha maisha bora kwa kila mwananchi.

Wakiongea na Mwandishi Wetu, wakazi wa Jiji la Arusha  wanabaisha wanavyonufaika na upatikana wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo nishati ya umeme katika maeneo yao, zahanati na vituo vya afya na ujenzi wa shule na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kazi kubwa inayofanya.

Laisi Masanja anayejishughulisha na biashara ya kinyozi katika eneo la Oljoro katika Kata ya Laroi Wilayani Arumeru anasema kupitia kazi hiyo ameweza kuhudumia familia yake bila tatizo lolote sanjari na kusomesha watoto wake.

Kwa upande wake Zaituni Saidi, mkazi wa Kijiji cha Enjoro anasema ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo umewasaidia kupata huduma za matibabu kwa karibu na kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo na wakati mwingine wagonjwa walikuwa wakifariki njiani kabla ya kufika hospitalini.

" Mbali na ujenzi wa kituo cha afya hapa kijijini lakini pia maisha yamekuwa rahisi baada ya kupata nishati ya umeme kupitia mradi wa REA kwa kuwa kina Mama wengi wameweza kuanzisha biashara ya saluni ya kike na kusaidia kutotembea umbali mrefu tena hadi moromboo au mjini kabisa kufuata huduma ya saluni," amesema Zaituni.

Namnyaki Mollel anasema kabla ya ujio wa umeme wa Rea katika kijijini cha Oloirien walikuwa wakitembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 50 kwenda kusaga mahindi kupata unga wa chakula lakini umeme umesaidia kuanzishwa kwa mashine na kupata huduma hiyo kwa karibu zaidi.

Ujumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ukikagua moja ya madarasa yaliyojengwa Wilayani humo 

Kwa upande wake Lomnyaki Zefania ameiomba Serikali kusaidia kuhamasisha wawekezaji kufika katika kijiji chao kuwekeza viwanda mbalimbali Ili vijana wa eneo hilo waweze kupata ajira kufuatia kuwa na umeme wa uhakika.

Isaria Ndaskoi, mkazi wa Olokii amesema ujenzi wa shule na ukarabari wa madarasa shule ya msingi Olokii umesaidia watoto wao kwenda shule kwa karibu na kuepukana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.i

Kivuko katika kijiji cha Laroi ambacho baada ya kujengwa wananchi WA kijiji hicho wamekuwa wakipita bila shida ikiwemo wanafunzi kwenda shule tofauti na hapo mwanzo, mvua zilipo nyesha mawasiliano ya pande zote yalikatika Kwa muda

" Watoto wengi walikuwa wakiacha shule kwa kuwa walikuwa wakitembea umbali mrefu hadi kufika shule na wakati mvua ikinyesha hapa jirani kuna korongo linajaa maji na kuzuia watoto wasiende shule mpaka mvua zikatike, lakini baada ya kujengwa kwa shule pamoja na kivuko cha uhakika sasa hivi watoto wanasoma na hakuna anayefikiria kuacha shule," amesema Ndaskoi.

Matumizi ya nishati safi ndio ajenda inayosisitizwa  kwa sasa na serikali ya awamu hii chini ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa watanzania wote.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post