NSSF ARUSHA YAJIVUNIA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE.

 

Na, Egidia Vedasto, 

APC Media, Arusha. 


Kuelekea kilele cha wiki ya huduma Kwa wateja, Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) Jijini Arusha umedai kujivunia kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuwaahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa zaidi wa utoaji huduma kwa kutumia mifumo ya kidijitali. 


Akifungua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, Mkurugenzi mkuu wa NSSF nchini Masha Mshomba amesema huduma bora kwa wateja ni suala litakaloendelea kupewa kipaumbele kuhakikisha wanafikia lengo la mfuko. 


"Tumefikia asilimia 97 kwa matumizi ya TEHAMA na tutahakikisha huduma zetu zinafika kila kona nchi nzima na kwa haraka", 


" Ni fahari kwetu  kuwafahamisha kuwa Juni 2025 tumefanikiwa kufikia mapato ya Trilioni 9.9, tunaamini ni kwa sababu ya ushirikiano wenu, katika mafanikio hayo shukrani zetu za dhati ziwaendee wadhamini wetu, Ofisi wa Waziri Mkuu na Benki Kuu, tunatamani ifikapo mwakani mfuko wetu ukue kufikia Tilioni 11.7" amesema Mshomba. 


Vilevile mfuko umeweza kuwafikia wateja waliojiajiri ambao ndio wengi kwa takwimu nchini, wameendelea kujiunga na mfuko na  wataweza kupata mafao ya uzeeni, mafao ya uzazi kwa wanaojifungua, matibabu na huduma nyingine nyingi katika maisha. 


Hata hivyo katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi kwa kila mtu ifikapo 2030, ambapo majiko takriban 100 yametolewa kwa waeja wakiwemo wastaafu. 


Kwa upande wake Meneja NSSF mkoa wa Arusha Josephath Komba ametoa shukrani zake kwa wadau wote kujumuika nao katika siku hiyo muhimu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, yaliyojumuisha waajiri, wafanyakazi wa mfuko, wananchama wanaojichangia kwa hiari na wastaafu. 


"Kipekee nawapongeza wafanyakazi wetu wa mfuko kwa kuchagua kaulimbiu ya " Kidigitali Tumeweza" iliyosaidia kurahisisha utekelezaji wa majukumu, sambamba na hayo tumefanikiwa waajiri wetu kulipa michango ya wanachama kupitia lango la NSSF linalofahanika kama "Lango Portal" na kwa asilimia miamoja wote wanalipa kwa njia hiyo" amesema. 


Vile vile ametaja changamoto kadhaa ambazo ni baadhi ya Waajiri kuchelewa kuwasilisha michango ya wananchama,  hatua inayolazimu kuwatembelea na kufanya mazungumzo kwa lengo la kulinda wananchama. 


Katika namna hiyo Robert Kadeghe meneja huduma kwa wateja NSSF amesema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka lengo likiwa ni kukutana na kutoa shukrani kwa wateja, kutoa tathmini ya mwenendo wa mfuko, kutambua mchango wa wanachama, kutambua wale waliofanya vizuri na kuwakumbusha wafanyakaz wa mfuko kutoa huduma bora.


Kadeghe amesema mfuko umewakumbuka wastaafu kuwa wanaweza kujihakiki kidijitali popote walipo pasipo kufika ofisi za NSSF, pia kupata maoni jinsi ya kuboresha huduma. 


"Tumedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja, tumejipanga kuhakikisha tunamaliza kero zinazowakumba  wateja wetu" amefafanua.


Mmoja wa wateja wa NSSF Martin Mollel amepongeza huduma bora zinazotolewa na mfuko wa NSSF, ikiwemo bima za afya. 


"Maombi yangu kwenu, naomba watoto wasitolewe katika mpango wa bima ya afya anapofikisha umri wa miaka 18, bali atakapofikisha miaka 22 maana naamini atakuwa ameweza kujitegemea mwenyewe, pia kwa upande wa wananfunzi wanaosoma nje ya Arusha kuwekwe utaratibu watibiwe hukohuko mikoani maana naamini NSSF iko kila mahali" amesema Mollel.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post