WAANDISHI WA HABARI WAPEWA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU


Na Mwandishi Wetu, Arusha

Tume ya Haki za binaadam na utawala Bora imewataka waandishi wa habari kutumia vizuri kalamu zao wakati wa kuripoti taarifa zao katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2025.

Akifungua mafunzo ya siku Moja kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, kaimu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mohamed Khamis Hamad amesema waandishi wa habari ni watu muhimu katika jamii hivyo taaluma hiyo inatakiwa kutumika vizuri.

Amesema waandishi wa habari wakitumia kalamu zao vibaya wataupotosha umma na kusababisha madhara makubwa kwa jamii ikiwemo kuleta machafuko ambayo matokeo yake ni kurudisha nyuma uchumi wa nchi jambo ambalo sio sahihi. 

Kwa upande wake mtoa mada katika mafunzo hayo Mohamed Bakari amesisitiza waandishi kuwa makini na kuzingatia sheria na taratibu, miiko na maadili katika utendaji kazi wao. 

"Katika kipindi hiki muhimu waandishi wa habari wana wajibu wa kuhamasisha wananchi kupiga kura, kama Ibara yq 21 kifungu cha (1-2) inavyobainisha kuwa ni haki ya kila raia kushiriki uchaguzi. Epukeni upendeleo, usiri wa mtu pamoja na kumpiga picha mpiga kura katika chumba cha kupigia kura" Amesisitiza Bakari. 

Mwandishi wa habari wa kituo ch Star TV na Radio Free Afrika aliyeshiriki mafunzo hayo Angelo Mwoleka amesema kila mwandishi azingatie kwanza usalama wake kazini, usalama  wa nchi  miiko na maadili ya uandishi. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post