JUKWAA LA TATU LA UTEKEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI LAWANUFAISHA WADAU SEKTA YA MADINI.

Mambo wa kuchongea miamba

 Egidia Vedasto 

Arusha 

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeongeza motisha na kiwango cha ubora katika utoaji huduma kwa Wadau wa Sekta ya Madini kutokana na Mikutano mbalimbali ambayo imekuwa ikitoa elimu na kuimarisha ushirikishwaji wa Wadau wa Sekta hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa    Kampuni ya Geofields Tanzania Ltd inayofanya kazi za utafiti na uchorongaji Miamba Mhandisi Paul Masatu

Akielezea namna alivyonufaika na Jukwaa la Tatu la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Tanzania katika Sekta ya Madini, Eng Paul Masatu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Utoaji Huduma katika Migodi Tanzania upande wa  utafiti na uchorongaji (GEOFIELDS TANZANIA LTD), amesema kutokana elimu iliyotolewa katika jukwaa hili italeta  mapinduzi makubwa katika Sekta ya Madini na Wadau wake kwa ujumla.

"Shughuli zetu kubwa sisi ni wataalam wa kufanya utafiti kwa watu wanaotaka kuwekeza aidha wazawa au wageni  pia tunajihusisha na uchorongaji wa miamba, na kwa upande wa changamoto ni kawaida kwani kila biashara ina changamoto zake, hivyo tunapambana kuzitatua kila mmoja kwa namna yake na Wizara yetu inafanya kazi kubwa kuboresha mazingira yetu ya kazi" amesema  Eng.Masatu.

Katika namna hiyo hiyo, Makam  Mwenyekiti Chama cha Wachimba Madini Mkoa Ruvuma, Kassim Pazi amebainisha changamoto zinazowakumba Sekta ya Madini mkoani humo kuwa ni ubovu wa miundombinu ya barabara na umeme usio wa uhakika.

"Ombi langu kwa serikali iendelee kuleta mikutano kama hii, kwani tunanufaika, tunajifunza kupitia makampuni mbalimbali yanayoshiriki lakini pia tunaibua vizingiti ambavyo Wizara huvipatia ufumbuzi"amesema.

Pazi amebainisha madini yanayopatikana Mkoani humo kuwa ni pamoja na Dhahabu, Chuma, Makaa ya Mawe na mengine, na kuiomba serikali kuimarisha miundombinu hiyo  ambao ni mhimu kwa Sekta ya Madini.

Sambamba na hayo, Meneja wa Usimamizi na Uhaurishaji Teknolojia, Tume ya Sayansi na Teknolojia Dar es Salaam  Dkt.Erasto Mlyuka, amebainisha kuwa, kutokana na jukwaa hilo amejifunza ushirikishwaji wa wananchi kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Madini,  kwa Wajibu wa sayansi na teknolojia kwa makampuni yaliyopo kwenye eneo la madini, kuna uhitaji mkubwa wa teknolojia ya namna bora ya kuhaurisha, kwa maana ya  teknolojia inayotakiwa.

Aidha Dkt. Mlyuka ameongeza, Sekta ya Madini inahitaji mtandao mpana wa mashirikiano wa sekta ya fedha, utafiti na maendeleo kwa sekta inayotoa huduma kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

"Wadau wa bima wameeleza vizuri ni mhimu Makampuni 

yakahakikisha yanakata bima za aina mbalimbali ili kuepuka hasara zisizotarajiwa" amesema Dkt.Mlyuka.

Pia kwa upande wake Francis Mgaya Meneja masoko katika Kampuni ya kuuza kemikali za kuchenjua madini Geita, Kahama, chunya na Musoma, amesema elimu aliyoipata ni kubwa, itamnufaisha katika majukumu yake.

"Kipekee nawashukuru CRDB kwa kuwa tayari kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo, na wakubwa na elimu ya kukata  bima ya mitambo na watumishi kwa ujumla"amesema.


Mkutano huo wa Jukwaa la Tatu la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini Jijini Arusha umedumu kwa siku tatu na kubeba kaulimbiu "Uwekezaji wa Viwanda vya Uzalishaji wa Bidhaa za Migodini kwa Maendeleo Endelevu".

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post