CRB KUANZISHA OPERESHENI UKAGUZI WA MIRADI MIKUBWA INAYOTEKELEZWA NA WAKANDARASI WA KIGENI

Msajili wa Bodi ya Makandarasi  Tanzania (CRB) Mhandisi Rhoben Nkori.

Egidia Vedasto 

Arusha.

Makandarasi wa ndani wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kujifunza nidhamu ya fedha ili kuepuka kushindwa kumalizia miradi wanayopewa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Arusha wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo makandarasi hao, Meneja wa Kanda ya Kaskazini Bodi ya Makandarasi QS Sauda Njila amesema mafunzo hayo yamewakutanisha Makandarasi takribani 150 kutoka nchi.

Njila amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuaminiwa na kupewa miradi mikubwa ambayo hapo awali ilikuwa ikitekelezwa na makandarasi kutoka nje ya nchi pamoja na kukuza uchumi wao tofauti na hapo awali.

"Mafunzo haya ya leo tunayoyapata yanalenga hasa kujua namna ya kutunza nidhamu ya pesa, unajua biashara yoyote inahitaji uelewa kwa mfano, mafunzo haya yataongeza uelewa katika kuipangilia pesa na kuweza kupanga bajeti  badala ya kutumia pesa za mradi bila maarifa na mpangilio na mwishowe kuikimbia miradi kabla ya kukamilika kutokana na pesa kuisha" ameeleza Njila.

Kwa upande wake Mhandisi Yahaya Mnari kutoka Kampuni ya Sahara Sareh Limited in Building and Civil Contractor Classified Dar es salaam, kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa Makandarasi watoa huduma shirikishi Tanzania (TOKASA) amesema mafunzo haya yametolewa  na Bodi ya Makandarasi na yanayolenga kuwaelimisha juu ya nidhamu ya pesa, kutunza muda, kuongeza muonekano wa kazi na kukuza uchumi kwa ujumla.

"Kabla ya haya mafunzo dosari zilikuwa zinaonekana sana, hali hii ndio ilikuwa inawapa nafasi wageni kupata miradi mikubwa na sisi tukibaki kuwa tegemezi  na kukosa nafasi nyingi za ajira na uchumi kuwa mdogo, na wenzetu wageni wakipata pesa wanapeleka kwao uchumi wao unapanda" amefafanua Mnari.

Mgeni rasmi aliyefungua mafunzo hayo, Msajili wa Bodi ya Makandarasi Tanzania (CRB) Mhandisi Rhoben Nkori, amesema kwamba Makandarasi wa kigeni wamekuwa wakipata miradi michache ila ikionekana kuwa na kiwango bora zaidi, lakini kwa sasa kuna mabadiliko kwani kumekuwa na malalamiko kuwa kuna baadhi ya  Makandarasi wageni wanatekeleza miradi chini ya kiwango tofauti na ilivyozoeleka.

Mhandisi Nkori amewataka Makandarasi waliobahatika kupata mafunzo hayo kutumia fursa hiyo vizuri kwani itawasaidia kutekeleza miradi mikubwa kutokana na kijifunza kwa wageni jinsi ambavyo wamekuwa wakitenda kazi.

"Hata katika ziara za Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, anasema kwamba amekuwa akibaini mapungufu makubwa kwa Makandarasi wa kigeni na kudai hali hii haitakubalika, hivyo amewasihi kutumia elimu mnayopewa ambayo itawasaidia kupambana na kuwa kama wao" amesisitiza  Mhandisi Nkori.

Amewasisitiza kufanya kazi kwa ufasaha pindi watakapopewa mikataba ya miradi mikubwa ili kuaminika na kujijengea jina zuri katika utaalam huo.

"Pia nataka tujifunze changamoto wanazopitia Makandarasi wageni ili kujua mbinu za kuteka soko, lakini pia kuna mpango wa kupitia sheria upya ili kuwabaini Makandarasi wageni wanaotenda kazi chini ya kiwango ili kutoa taarifa mahali panapohusika na hatua sahihi za kufutiwa usajiri wa ukandarasi zitachukuliwa" ameongeza Mhandisi Nkori.

Mkutao huo wa mafunzo unaofanyika Jijini Arusha utadumu kwa siku tatu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post