CLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA ( SPC ) YAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, RC MACHA APONGEZA

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Greyson Kakulu akisoma risala leo Mei 15,2024.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club) SPC leo Meo 15,2024 imeadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani huku ikihamasisha jamii kutunza mazingira ili kusaidia  utekelezaji wa mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034.

Hafla ya maadhimisho hayo imefanyika katika ukumbi wa mikutano Karena Hotel na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi binafsi, vyama vya kisiana, wadau pamoja na baadhi ya wananchi ambapo mgeni rasmi ni mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

Akisoma risala, Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Greyson Kakulu pamoja na mambo mengine amesema klabu hiyo imejipanga kikamilifu katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira ili kusaidia  utekelezaji wa mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034.

Mwenyekiti huyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi hizo huku akisisitiza  ushirikiano katika maeneo ambayo waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga watayafikia ikiwa ni sehemu pia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Tunaposherekea maadhimisho ya Mwaka huu, vyombo vyetu vya habari vinaweka mtazamo juu ya mabadiliko ya tabia nchi kwa nia kubwa ya kutoa elimu kwa jamii itakayochochea uhifadhi na utunzaji wa mazingira”.

“Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu “uandishi wa habari na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi” ndugu wadau wa habari: tunahitaji ushirikiano wa dhati kutoka kwenu kwa ajili ya kampeni ya mazingira ndani ya mkoa wetu “NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA YA MABADILIKO YA TABIA NCHI, kampeni hii itaendeshwa na vyombo vyetu vya habari kupitia majukwa mbalimbali ili kuhamasisha jamii yetu kutunza mazingira, kampeni hii  itasaidia pia utekelezaji wa mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034”. amesema Mwenyekiti Kakulu

“Ndugu wadau wa habari Waandishi wa habari wanahitaji ushirikiano kutoka kwenu juu ya habari za mazingira kwa taasisi zote za umma na binafsi katika kutoa elimu na hata maeneo mengine, Mkoa wetu kwa mwaka 2022 kwa taarifa kutoka Baraza la Habari Tanzania, ulishika nafasi ya 02 kwa wanahabari kufanyiwa madhira mbalimbali ikiwa ni kunyimwa taarifa kutoka ofisi za umma na binafsi na hii ilifanya jamii kukosa haki ya habari kwa maeneo tofauti”.

“Ndugu wadau wa habari Uhuru wa kujieleza ni uhuru wetu sote bila aina yoyote ya ubaguzi,Niki mnukuu Katibu wa Umoja wa Mataifa ,Antonio Guteress (Mei 3,2023) ,alisema, Uhuru wetu wote unategemea uhuru wa vyombo vya habari. Tunasomo kubwa la kujifunza juu ya UVIKO-19, kama vyombo vya habari tungekaa kimya,wengi wetu hapa tusingekuwa hai hadi leo. Hivyo basi usalama kwa maeneo yote ni uhuru wa vyombo vya habari”.

“Ndugu wadau wa habari Nawashukuru sana kwa kutupa ushirikiano kwa vyombo vya habari kwa mwaka 2023 na mkoa wetu haukuweza kuwa na madhira mengi kama ilivyokuwa huku nyuma kwa matu”. amesema Mwenyekiti Kakulu

SPC kupitia Mwenyekiti wake Greyson Kakulu imeishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya marekebisho ya sheria ya kifungu 09 ya sheria ya vyombo vya habari pamoja na kuongeza uhuru wa kujieleza ambayo pia hivi karibuni itatekeleza mradi wa UHURU WA KUJIELEZA.

“Ndugu wadau wa habari Tunashukuru serikali ya awamu ya sita, Mhe.Dkt Samia suluhu kwa kufanya marekebisho ya sheria ya vifungu 09 ya sheria ya vyombo vya habari na kuongeza uhuru wa kujieleza”.

“Hivi karibu klabu yetu itakuwa na mradi UHURU WA KUJIELEZA ambao utakutanisha kupitia majukwa mbalimbali kwa ajili tena na tutajadili mambo mbali kwa ajili ya masilahi ustawi wa mkoa wetu, Mradi huu utawapa haki kwenu kama wadau kupaza sauti juu ya ustawi wa maendeleo ya mkoa wetu katika majukwa mbalimbali”.amesema Mwenyekiti Kakulu

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewahakikisha waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuendelea kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao huku akiwapongeza kwa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari 2024.

Pia amesisitiza watendaji wengine wa serikali, taasisi binafsi pamoja na wadau  mbalimbali katika  Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari ili jamii iweze kufahamu changamoto na maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

RC Macha amewahimiza waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutumia kalamu zao vizuri na kutekeleza utekelezaji wa majukumu yao unazingatia  sheria na taratibu zilizopo ili kuepusha migogoro na upotoshaji katika jamii.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi halali huku akiwaomba waandishi wa habari kuhamasisha jamii kufanya kazi halali ili kuinuka kiuchumi na  kuepukana na hali utegemezi.

Amewataka waandishi wa habari kuandika Habari kwa kuzingatia Misingi na Kanuni za uandishi wa Habari hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji 

Katika maadhimisho hayo ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari viongozi na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wameshiriki kujadili  mada mbalimbali ikiwemo umuhimu wa vyombo vya habari katika habari za mazingira, uharibifu wa mazingira na athari kwa wanawake na watoto pamoja na ukatili wa kijinsia.

Kila mwaka jamii ya wanahabari dunia huwa na tabia ya kufanya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari dunia kila Mei 3 na klabu za habari kote Tanzania kupanga ratiba ya kukutana na wadau wake ndani ya mikoa katika Mwezi Mei ya kila mwaka ambapo klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) imeadhimisha leo Mei 15, 2024.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwapongeza waandishi wa habari Mkoa huo kwa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari. 

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Greyson Kakulu akisoma risala leo Mei 15,2024.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha awali akiwasili ukumbini huku akiongozwa na Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakulu.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikabidhi miche ya miti uliyoandaliwa na SPC ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kauli mbiu ya siku ya maadhimishi ya uhuru wa vyombo vya habari inayosema “uandishi wa habari na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi”.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikabidhi miche ya miti uliyoandaliwa na SPC ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kauli mbiu ya siku ya maadhimishi ya uhuru wa vyombo vya habari inayosema “uandishi wa habari na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi”.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikabidhi miche ya miti uliyoandaliwa na SPC ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kauli mbiu ya siku ya maadhimishi ya uhuru wa vyombo vya habari inayosema “uandishi wa habari na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi”.

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post