TIMU 16 KUWANIA UBINGWA WA JAMUKAYA RAMADHANI CUP 2024 UWANJA WA SHY COM MKOANI SHINYANGA.

 Na Elisha Petro 

Michuano ya Jamukaya Ramadhani Cup msimu wa 2024 inatarajia kuanza kutimua vumbi  katika uwanja wa SHYCOM uliopo Mkoani Shinyanga kwa timu 16 kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Meneja rasilimali watu,utawala na sheria wa Jambo group  Wakili John Palamagamba Kabudi amebainisha kuwa jumla ya shilingi million 2 zimetengwa kwa ajili ya mshindi wa kwanza,wapili na watatu huku lengo la mashindano hayo ni kusaidia watu wenye uhitaji wakiwemo wajane na watoto yatima.

Wakili John amesisitiza kuwa upatikanaji wa timu zitakazoshiriki ni kupitia usajili unaoendelea kufanyika katika ofisi za Jambo FM (Ibadakuli) kwa timu mbalimbali za mitaani na taasisi kwa gharama ya shilling laki mbili na nusu (Tsh 250,000)  na kujipatia seti ya jezi bure.

Sambamba na hayo, waakili John amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi kwani kiingilio ni shilingi 500 ambapo kila shabiki atapatiwa kinywaji cha bure  kwa kila mchezo.

Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 14/3/2024 kuanzia saa 3:15 usiku hadi tarehe 3/4/2024.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post