SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA YAKUTANA, KUZUNGUMZA NA SHIRIKA LA THUBUTU AFRICA INITIATIVES

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya viongozi wa kampeni ya kupinga ukatili Nchini SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga leo wamekutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives Bwana Jonathan Kifunda Manyama.

Viongozi hao pamoja na mambo mengine kwa pamoja wameazimia kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao hasa ya kupambana na vitendo vya ukatili huku Mkurugenzi Bwana Manyama akiipongeza kampeni hiyo ya SMAUJATA kwa namna viongozi wanavyojitoa katika kuibua vitendo vya ukatili.

Bwana Jonathan Manyama pia ni Mwenyekit wa mtandao wa kupinga na kuzuia vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga ( SHY-EVAWC)

Thubutu Africa Initiatives ni Shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza miradi katika maeneo matano (5) ambayo ni AFYA, ELIMU, HAKI ZA BINADAMU, MAZINGIRA na MASHIRIKIANO na Taasisi zingine.

Shirika hilo ambalo linatakribani Miaka kumi linatekeleza miradi katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini ikiwemo Mkoa wa  Mwanza, Shinyanga, Tabora, Morogoro pamoja na Njombe.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambao wameshiriki kikao hicho leo ni katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya, Mwenyekiti idara ya jinsia SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Inspekta Alkwin Willa pamoja na Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Kishapu Bwana Emmanuel Makolo.

Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini ambayo ipo Mikoa yote  inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

Kauli mbiu ya kampeni hiyo inasema “KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA”

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wameendelea na ziara, kutembelea na kuzungumza na taasisi mbalimbali zikiwemo za Dini na taasisi na Serikali na binafsi ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano katika utekelezaji wa makumu yao kwa lengo la kutokomeza ukatili unaoendelea kufanyika kwenye jamii.

Baadhi ya viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Thubutu Africa Initiatives Bwana Manyama leo Machi 27,2024.


 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post