KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAWASILI SHINYANGA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MIWILI YA MAENDELEO


Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu leo Machi 14,2024 imefanya ziara Mkoani Shinyanga ambapo imetembelea na kukagua Mkongo wa Taifa katika shirika la  mawasiliano Tanzania (TTCL) mjini Shinyanga pamoja na mradi katika ukarabati na uboreshaji wa kiwanja cha Ndege cha Shinyanga kilichopo kata ya Ibadakuli.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa mawasiliano Shinyanga mjini mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la mawasiliano Nchini TTCL Peter Ulanga amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa ulianza Mwaka 2009, ukiwa na uwezo wa 40G na badae kuongezeka uwezo kuwa 200G.

Ameeleza kuwa katika awamu hii uwezo wa mitambo umeongezeka kutoka 200G mpaka 800G ambapo tayari mitambo hiyo inafanya kazi kwa Singida – Shinyanga – Mwanza na Shinyanga – Kahama na kwamba ujenzi bado unaendelea katika maeneo mengine.

“Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa ilianza Mwaka 2009, ikiwa na uwezo wa 40G na badaye kuongezwa uwezo kuwa 200G na badaye kuongezwa uwezo wa 400G kwa Singida – Shinyanga – Mwanza  ujenzi wa awamu hii umeanza toka 2021\2022 maeneo mbalimbali ikiwa pamoja na Mkoa wa Shinyanga, ujenzi  wa Mkongo wa Taifa Mkoani Shinyanga umejikita katika maeneo makuu mawili ambayo ni usimikaji wa mitambo na ujenzi wa nguzo za zege sambamba na uvutaji wa Waya za Faiba”.

“Katika awamu hii uwezo wa mitambo umeongezwa kutoka 200G MPAKA 800G na tayari mitambo inafanyakazi kwa Singida – Shinyanga – Mwanza, na Shinyanga – Kahama na ujenzi unaendelea maeneo mengine”.amesema Peter

Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Mhe. Nape Mnauye amesema Wizara hiyo inaendelea kuboresha miundombinu ya mawasiliano ambapo Mkongo ni moja ya njia ya mawasiliano ya kimtandao.

Duniani inakwenda kwenye uchumi wa kidigtali uchumi huu unatumia Barabara kubwa na ndogo lakini zenyewe ziko kwenye ulimwengu wa mtandao na kazi yetu nikutendeneza miundombinu kwenye ulimwengu wa kimtandao ili watu wawasiliane wabadilishane bidhaa muuzaji na mnunuzi wakutane kwenye ulimwengu wa kimtandao na ili wakutane wanahitaji miundombinu ya kimtandao na ndiyo maana tunajenga Mkongo mkubwa na tunajenga pia na Mikongo midogo lakini pia tunajenga Minara ambayo yote kwa pamoja lengo lake moja tu kuwafanya watu na taasisi ziweze kuzungumza ziweze kusomana ziweze kuwasiliana ziweze kufanya biashara  kwahiyo kwa kifupi Mkongo ni Barabara ya mawasiliano ya kimtandao”.amesema Waziri Nape

Kamati ya kuduma ya Bunge ya miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti yake  ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Mhe. Seleman Moshi Kakoso imeipongeza Wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari kwa ubunifu huo huku wakiisisitiza TTCL kuusimamia Mkongo wa Taifa huo ili uweze kujiendesha  kibiashara kwa kuwa unatoa huduma zinazoingiza Fedha.

“Kamati ya Bunge ilipambana kuhakikisha TTCL mnaumiliki Mkongo wa Taifa sasa tunachowaomba mkisimamie msije mkawa mnategemea ile ruzuku ya Serikali sisi tunataka Mkongo wa Taifa ujiendesha kibiashara kwa sababu mnatoa huduma ambazo zinaleta Fedha nyingi mnapelekea huduma Burudi, Rwanda, Kenye na kwingineko lakini pia ndani ya Nchi hum tunaomba mkae ukiwemo wewe Mkurugenzi uhakikishe unakuwa mbunifu mnausimamia huo Mkongo ili uweze kujiendesha kibiashara”.amesema Mhe. Kakoso

Aidha Kamati ya kuduma ya Bunge ya miundombinu wakati ikitembelea na kukagua mradi katika ukarabati na uboreshaji wa kiwanja cha Ndege cha Shinyanga imepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika Oktoba 3,2024.

Katika taarifa yake kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Dorothy Mtenga amesema hadi sasa mradi umefikia asilimia 11,02 ambapo tayari umetoa jumla ya ajira 115 kati ya hizo, ajira 100 sawa na asiliamia 87 zimetolewa kwa watanzania.

Amesema baada ya kukamilika kwa meadi huo utarahisisha usafiri kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga, Simiyi na mikoa ya jirani pia utarahisisha shughuli za kibiashara hasa Madini, ufugaji na Kilimo.

Ametaja faida zingine kuwa, mradi huo utarahisisha shughuli za kijamii, utaguza uchumi wa Mkoa wa Shinyanga na Simiyu lakini pia utasaidia shughuli za utafiti wa Kilimo pamoja na kusaidia kukuza utalii wa Mkoa wa Shinyanga Mikoa jirani na Taifa kwa ujumla.

Mhandisi Dorothy ametaja hatua mbalimbali zilizokamilika katika mradi huo ikiwemo Barabara ya kuruka na kutua Ndege (Ruwey) asilimia 40.3 pamoja na uhamishaji wa miundombinu ya Maji, Umeme na mawasiliano kwenye eneo la ujenzi.

“Hadi sasa mkandarasi amekamilisha kazi ya ujenzi wa ofisi ya Mhandisi mshauri kwa asilimia mia moja (100), amekamilisha Barabara ya kuruka na kutua Ndege (Runway) kwa asilimia 40.3, Maegesho (Apron)  asilimia 40, Barabara ya kiungio (Taxiway) asilimia 40, ujenzi wa Contactors Camp mitambo ya kufanya kazi asilimia mia moja (100), kusafirisha eneo la jingo la Abiria asilimia mia moja (100)”.

“Lakini pia mkandarasi kazi zingine zilizokamilika ni kusafisha eneo la maegesho ya Magari asilimia mia moja, kusafisha eneo la ujenzi wa uzio asilimia kumi (10) uchimbaji wa msingi wa jingo la Abiria asilimia mia moja, ujenzi wa msingi wa jingo la Abiria asilimia 90, ujenzi wa jingo la Abiria asilimia 15, vifaa vya ujenzi(Materials) asilimia 80, kuagiza vifaa vya uendeshaji wa jingo vyenye kuchukua asilimia 50 ya maendeleo ya ujenzi ni asilimia 30, ujenzi wa Nguzo asilimia mia moja, ujenzi wa Tenki la kuhifadhi maji asilimia tano (5), ujenzi wa eneo la kuegesha Magari asilimia 35 pamoja na ujenzi wa formworks kwa ajili ya ghorofa ya kwanza umefikia asilimia 45”.amesema Dorothy

Baada ya kamati ya kuduma ya Bunge ya miundombinu kutembelea na kukagua mradi huo Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Seleman Moshi Kakoso ametoa maelekezo mbalimbali ikiwemo suala la CSR pamoja na kuhakikisha mkandarasi atatekeleza wajibu wake ili kukamilisha mradi kwa wakati.

“Jambo la kwanza Serikali inawataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo haya mradi huu uweze kuwanufaisha wapate CSR jambo la pili ni kumsimamia mkandarasi atimize wajibu wake afanye kazi kwa wakati mradi uendane sambamba na mkataba aliosaini pamoja na ufanisi wa kazi jambo la mwisho tunamuomba mkandarasi aweze kuwatumia vijana wa kitanzania kwenye maeneo wanayofanya kazi lakini waweke usawa juu ya malipo kwahiyo haya yakitekelezwa mradi utaenda vizuri na utaweza kuwasaidia watanzania”.amesema Kakoso

Ukarabati wa kiwanja cha Ndege Shinyanga awamu inayoendelea unafadhiliwa kwa fedha ya mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank – EIB).
 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post