Breaking News: Ajali mbaya, 40 wasadikiwa kufariki

Gari inayoelezwa kusababisha ajali baada ya kufeli breki.
Wakazi wa Kibaoni wakishuhudia gari la kunyanyua mizigo (Crane), ikijaribu kunyanyua magari yaliyogongwa ili kutoa miili ya abiria na majeruhi iliyoko ndani ya magari hayo 

 Na Seif Mangwangi,

Arusha

Zaidi ya watu 40 wanasadikiwa kufariki Dunia katika ajali ya gari iliyoshirikisha gari la wanafunzi aina ya costa namba T673DEW mali ya shule ya New Vision , daladala inayobeba abiria kati ya Arusha na Ngaramtoni, gari binafsi aina ya benzi na gari la kubeba mizigo lenye namba za usajili za nchini Kenya.

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa ajali hiyo imetokea  majira ya saa10 jioni katika Kijiji Cha Oloirieni eneo la Kibaoni, Ngaramtoni barabara kuu ya Arusha -Namanga baada ya gari la mizigo aina ya scania yenye tela namba za usajili KAC 943H la nchini Kenya kufeli breki na kugonga magari hayo matatu.

Mashuhuda wa tukio hilo wameieleza APC Media kuwa gari la wanafunzi kilikuwa limebeba wamiliki wa shule ya New Vision raia wa Korea pamoja na walimu ambao ni Watanzania ambapo walikuwa wakitokea katika kikao shuleni na kwamba wakiwa katika kituo Cha daladala Kibaoni gari la abiria lilikuwa limesimama kupakia abiria ndipo Lori hilo la mizigo lilipowavaa kwa nyuma.

Abiria katika gari hilo la wanafunzi pamoja na benzi wanaelezwa kufariki wote huku abiria wawili katika daladala wakiwa wametoka wazima na kuwahishwa hospitali kwa matibabu

Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari lililokuwa limepakia mtambo wa mashine ya kutengeneza barabara kuacha njia na kuparamia magari matatu ambayo ni Coster,Haice na gari binafsi lililokuwa imepakia raia wa kigeni ambao wawili kati yao wanahofiwa kufariki dunia eneo la tukio.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya Rufaa Mt Meru ,huku majeruhi wakipelekwa kupatiwa matibabu katika hospitali ya ALMC na Mount Meru

Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kutoka Mamlaka za Kiserikali hususani kuhusu idadi kamili ya waliofariki.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post