RUWASA MKOA WA SHINYANGA WAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAJI WILAYA YA KISHAPU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa viti maalum kupitia CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba leo Jumatano Novemba 29,2023 amefanya ziara ya Wilaya ya Kishapu kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga.

Katika ziara hiyo Mhe. Kirumba ameambatana na viongozi wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Mkoa wa Shinyanga wakiwemo viongozi wa UWT kutoka kwenye Halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga.

Viongozi hao wametembelea  ujenzi wa mradi wa maji ya ziwa Viktoria Seseko - Ngundangali unaotekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu kupitia mradi wa P4R mradi huo unatekelezwa kwa muda wa mwaka  mmoja na  unatarajiwa   kukamilika  Mwezi Machi,  2024.

Akisoma taarifa fupi ya mradi huo wa maji ya Ziwa Viktoria Seseko – Ngundangali, meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu mhandisi Dickson Kamazima amesema mradi huo utawanufaisha wananchi katika vijiji vitano vya kata ya uchunga Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

Katika ziara hiyo pia wametembelea ujenzi wa mradi wa maji kata ya Igaga ambao thamani yake ni shilingi Bilioni 6.6 na kwamba mradi huo utawanufaisha wananchi wa vijiji 13.

Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wamesema kukamilika wa miradi ya Maji inayotekelezwa na wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga itasaidia kumaliza changamoto wanazokutana   nazo.

Wamesema wamekuwa wakitumia Maji ambayo si salama hali inayohatarisha usalama wa Afya zao na kwamba ubali mrefu wa maji unasababisha migogoro kwenye familia ikiwemo ukatili wa kijinsia ambapo wameishukuru serikali kupitia RUWASA Mkoa wa Shinyanga kwa kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama.

Mbunge wa viti maalum kupitia CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba ameipongeza RUWASA Mkoa wa Shinyanga kwa kasi nzuri ya utekelezaji wa Miradi huku akiwaomba wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuendelea kutatua changamoto zilizopo.

 Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphance Butondo amesema miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA Mkoa wa Shinyanga katika jimbo hilo baada ya kukamilika upatikaji wa maji utakuwa zaidi ya asilimia 65 na kwamba amewapongeza viongozi wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa miradi hiyo.

Kwa upande wake meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela ameeleza kuwa miradi yote ya Maji inayotekelezwa na RUWASA Mkoani Shinyanga itakamilika kwa wakati pamoja na kuwapa vipaumbele wananchi wazawa kwenye suala la ajira.

Mbunge wa viti maalum kupitia CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba na meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela upande wa kulia baada ya kuwasili katika kata ya Uchunga kwa ajili ya kutembelea mradi wa maji leo Jumatano Novemba 29,2023.
This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post