MAFUNZO KWA VIONGOZI WA MATAWI TUGHE MKOA WA SHINYANGA WATUMISHI WA UMMA WAKUMBUSHWA MAMBO MUHIMU IKIWEMO NIDHAMU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Chama cha wafanyakazi wa serikali na Afya Tanzania TUGHE Mkoa wa Shinyanga kimefanya mafunzo kwa viongozi wa matawi leo Jumatano Novemba 22,2023  yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka kwenye taasisi za umma.

Awali akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Baraza kuu Taifa (KUBK) Dkt. Allan Masanja amewakumbusha watumishi wa umma kuendelea kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.

Mwenyekiti huyo amesisitiza watumishi wa umma kuwa na nidhamu na kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kujiepusha na migogoro kwenye sehemu za kazi.

“Usimamizi wa nidhamu ni suala muhimu kwa ustawi wa taasisi za umma na serikali kwa ujumla, bila kuwa na watumishi wenye nidhamu nzuri haitakuwa na maana hata wakiwa na uwezo mkubwa kiutendaji, hivyo ni wajibu wetu watumishi wa umma kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazotuongoza kwani nidhamu ni upande wa pili wa shilingi ya ufanisi katika kazi”.amesema Dkt. Allan

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga , Ramadhani Pangara pamoja na mambo mengine amewataka watumishi wa umma kujiepuka na makosa yanayopelekea kuondolewa kazini ikiwemo kutenda au kuwa na dhamira ovu ya kufanya vitendo viovu kama vile vitendo vinavyohusu Rushwa na wizi.

Ametaja makosa mengine yanayoweza kusababisha kuondolewa kazini ambayo ni kumdharau mwajiri, utoro kazini kwa muda wa zaidi ya siku tano bila ruhusa au sababu za msingi, uzembe unaosababisha hasara kwa mwajiri pamoja na kukataa au kukaidi kwenda katika kituo cha kazi alichopangiwa.

“Watumishi tuepuke kutenda au kuwa na dhamira ya kufanya vitendo viovu vinavyodhalilisha utumishi wa umma, kutumia bila kibali au idhini ya mamlaka halali mali au vifaa vya umma kwa manufaa binafsi, kujihusisha na kazi au shughuli yoyote nje ya kazi za kiofisi kwa kutumia wadhifa au cheo kinyume na maslahi ya umma lakini pia kosa la mtumishi kushindwa kutekeleza ipasanyo majukumu yake anaweza kuondolewa kazini, kutoa taarifa za siri kinyume na sheria ya usalama wa Taifa sura ya 47, kutenda au kuwa na dhamira ya kutenda jambo kinyume na maslahi ya umma, kushindwa kutekeleza majukumu kwa ufasaha au ukamilifu kutokana na matumizi ya Pombe au madawa ya kulevya”.

“Makosa mengine ni uzembe uliokithiri katika kutekeleza majukumu yako, ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma na maadili ya viongozi wa umma, kutenda makosa mepesi mara nne mfululizo, kutenda au kuwa na dhamira ovu ya kufanya matendo yanayokiuka sheria serikali mtandao naya uhalifu wa kimtandao na ile inayohusu masuala ya uhujumu uchumi, kutenda au kuwa na dhamira yakufanya matendo yanayokiuka sheria ya masuala ya Rushwa sura 329 pamoja na kutenda au kuwa na dhamira ovu ya kufanya matendo yanayokiuka sheria ya kupambana na kuzuia madawa ya kulevya ya sura 95 haya ndiyo baadhi ya makosa yanayoweza kusababisha mtumishi afukuzwe kazini”.amesema Pangara

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga Ramadhani Pangara ameelezea mambo mbalimbali kwenye mafunzo hayo ikiwemo dhana ya usimamizi wa nidhamu, amefafanua kuhusu mamlaka za nidhamu, mwenendo wa hatua za nidhamu au taratibu za kuendesha nidhamu, changamoto, masharti ya lazima ya kisheria ya kuzingatia pamoja na mambo ya kuzingatia kwenye hati ya mashtaka huku naye akisisitiza watumishi wa umma kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa ambaye pia ni afisa muuguzi msaidizi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Experantia Misalaba ameelezea kuhusu udhibiti wa magonjwa sugu yasiyoambukizwa mahali pa kazi katika utumishi wa umma.

Amesema magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo, Kisukari aina ya kwanza, mfumo wa hewa (Pumu) , magonjwa sugu ya kurithi, Macho, Figo, kuvimba tenzi ya shingo, magonjwa ya afya ya akili (kifafa), Saratani  pamoja na magonjwa ya misuli na mifupa.

Aidha katika semina hiyo imetolewa elimu na viongozi wa Public Service Social Security Fundi (PSSSF) juu ya mambo mbalimbali ikiwemo fomla ya kulipa mafao kwa watumishi wa umma (Kikokotoo) huku mwakilishi kutoka taasisi ya mfuko wa Taifa wa bima ya Afya akieleza faida za kujiunga na bima hiyo.

Baadhi ya viongozi wa matawi TUGHE Mkoa wa Shinyanga wameshukuru na kuwapongeza wawezeshaji katika mafunzo hayo ambapo wamesema elimu hiyo imewasaidia kuwakumbusha mambo muhimu ya kuendelea kuzingatia hasa sehemu za kazi huku wakiwaomba watumishi wengine kujiunga na chama hicho.


Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Baraza kuu Taifa (KUBK) Dkt. Allan Masanja akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Jumatano Novemba 22,2023 katika ukumbi wa Liga Hotel.

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga , Ramadhani Pangara akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi PSSSF baada ya mafunzo hay oleo Jumatano Novemba 22,2023.

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga , Ramadhani Pangara akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi PSSSF baada ya mafunzo hay oleo Jumatano Novemba 22,2023.

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga , Ramadhani Pangara akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi PSSSF baada ya mafunzo hay oleo Jumatano Novemba 22,2023.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post