CHAMA CHA TUGHE MKOA WA SHINYANGA CHAWAOMBA WATUMISHI WA UMMA KUJIUNGA ILI KUNUFAIKA NA FURSA ZILIZOPO

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali na Afya Tanzania (TUGHE)  Mkoa wa Shinyanga Dkt. Allan Masanja amewaomba watumishi wa umma ambao hawajajiunga na chama hicho waweze kujiunga ili kunufaika na fursa zilizopo.

Ameyasema hayo baada ya kushiriki kikao cha pamoja cha viongozi wa kamati tendaji TUGHE Mkoa wa Shinyanga ambapo amesema ni muhimu kila mtumishi mwenye sifa kujiunga na chama hicho na kwamba pamoja na mambo mengine chama hicho kinasaidia kuzuia migogoro ya wanachama katika sehemu zao za kazi.

Amesema zipo fursa mbalimbali wanachama wa TUGHE wananufaika nazo ikiwemo elimu mbalimbali za namna ya utekelezaji wa majukumu  sehemu za kazi katika kutimiza wajibu wa mfanyakazi, namna ya kupata mafao baada ya kustaafu , namna ya kujiandaa kustaafu pamoja na kutatua changamoto za wafanyakazi.

Dkt. Allan ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Baraza kuu Taifa (KUBK) ametumia nafasi hiyo kuwaomba watumishi wengine ambao bado wahajajiunga na chama cha TUGHE Mkoa wa Shinyanga, wajiunge ili waweze kunufaika na fursa zilizopo ndani cha chama.

“Tunapokuwa katika majukumu yetu ya chama kwanza tunawahamasisha wanachama wetu wajue umuhimu wa chama kinavyoweza kuwasaidia katika shughuli zao za kiutumishi wakiwa kazini, mahali pa kazi hata sehemu yoyote ile ambayo wao wanawajibika kama watumishi wa umma”.

“Kazi yetu ni kuhakikisha kwanza tunazuia migogoro ya wafanyakazi na mwajiri inayoweza kujitokeza aidha wakati mwingine mtumishi anaweza kufanya kosa bila kujua lakini chama kinaweza kumuelimisha majukumu yake na wajibu wake akiwa sehemu za kazi pamoja na hayo sisi ni kiunganishi tunapeleka hoja zetu kwa mwajiri ambazo watumishi wamezitoa sehemu za kazi kwa kutaka kuelewa stahiki na changamoto ambazo wafanyakazi wanazipata” amesema Dkt. Allan

“Mfumo wetu upo ndani ya matawi ambapo wanachama wanawasilisha changamoto zao ngazi ya matawi nao wanasiwasilisha ngazi ya Wilaya badae zinawasilishwa ngazi ya Mkoa tukishajadili ngazi ya Mkoa badae tunazituma ngazi ya Mkoa kwa ajili ya utatuzi”.

“Lakini mara tu mtumishi anapoingia kwenye mgogoro cha cha TUGHE kinawanasheria ambapo inapoonekana wanachama wetu ameingia kwenye kosa ambalo yeye hakutarajia au hakukusudia kulifanya anajikuta aidha anapelekwa Mahakamani au anasimamishwa kazi wanasherea wetu wa TUGHE wanamsaidia kutatua”.amesema Dkt. Allan

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati za wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa ambaye pia ni afisa muuguzi msaidizi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Experantia Misalaba amesema kupitia chama hicho wanawake wameendelea kuinuka kiuchumi kutokana na fursa zilizopo ikiwemo miradi mbalimbali wanayoiendesha.

Amesema miradi hiyo inawasaidia wanawake kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja ambapo naye  amewaomba watumishi wa umma wanawake Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenye  chama cha TUGHE ili kuendeleza umoja katika kutatua changamoto za wanawake.

Kikao cha pamoja cha viongozi wa kamati tendaji TUGHE Mkoa wa Shinyanga kikiendelea katika ukumbi wa mikutano Liga Hotel Manispaa ya Shinyanga.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post