WASTAAFU PSSSF KUTUMIA SIMU KUJIHAKIKI

Mkurugenzi wa Tehama Gilbert Chawe akisikiliza madai ya mstaafu Linus Ambrose Ngaida aliyekuwa mtumishi wa Halmashauri ya Karatu, ambaye mafao yake yamekosewa. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSSSF Venoss Koka.

 Na Seif Mangwangi, Arusha

MFUKO wa hifadhi ya Jamii wa PSSSF umewarahisishia wastaafu na waajiri wa mfuko huo huduma ya kusajili na kuhakiki mafao yao ambapo hivi sasa  watatumia mtandao wa Tehama kupitia mfumo wa PSSSF Kiganjani App badala ya kufuata huduma hizo ofisini.


Akizungumza Leo 5 Oktoba2023 katika ofisi za mfuko huo Jiji la Arusha ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja, Mkurugenzi wa Tehama wa mfuko wa PSSSF, Gilbert Chawe, amesema hivi sasa wastaafu hawatasumbuka kufika ofisi za PSSSF kujihakiki na badala yake huduma zote zinazohusu mafao watazipata mtandaoni.


"Ndugu zangu Leo tuko hapa kwaajili ya kuadhimisha wiki ya mteja, hata hivyo PSSSF ni wasikivu sana, katika semina zetu mlisema mnataka huduma Karibu, Sasa hivi mtazipata kupitia Simu janja, hutalazimika kuja ofisini kuhakiki mafao yako, kule kule ulipo utapata huduma, kikubwa Simu yako inatakiwa kuwa na Internet,"amesema Chawe.


wateja wa mfuko wa hifadhi ya Jamii PSSSF wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea ambapo Meneja Tehama wa Mfuko huo Gilbert Chewa aliendesha zoezi la kukata keki na kugawa miti ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya mteja 

Amesema kwa kutumia Simu janja huduma hiyo ya kielekroniki, itamtaka mstaafu kujisajili kabla ya kuanza kutumia na baada ya kujisajili itampatia maelekezo ikiwemo kufanya uhakiki kupitia vidole vya mkono wake.


" Mstaafu akishajisajili atatakiwa kupiga picha vidole vya mkono wake, na hapo hapo mawasiliano yatatufikia moja kwa moja na kwa kuwa mfuko una Mawasiliano na NIDA hakutakuwa na shida ya kutambua kama ni yeye kweli au la!...hii imekuja kurahisha na kuondoa usumbufu wa wastaafu kutembea makaratasi lakini pia imeondoa adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya kujihakiki, hata kama Uko nje ya nchi mafao yako utayapata,"Amesema.


Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini  Vonnes Koka, amesema mfuko umeanza kupeleka huduma Wilayani ambapo hivi sasa wafanyakazi wa mfuko watawahudumia huko huko kwa kutumia mashine ya Biometric ambapo mstaafu atatakiwa kuweka vidole vya mkono wake na taarifa zake zote zitafika ofisini.


Amesema tangu wiki ya mteja ilipoanza Oktoba 2, 2023 ofisi ya Mkoa wa Arusha imeweza kuhudumia zaidi ya wateja 500 ambao wengi wao walifika kwaajili ya uhakikina baadhi ya waajiri walifika kuleta mafao ya waajiri wao.


"Idadi ya wateja waliofika kupata huduma kuanzia Jumatatu ni zaidi ya 500 hata hivyo ni idadi ndogo kulingana na hapo nyuma na hii inachangiwa na huduma nzuri tunazotoa ikiwemo mfumo mpya wa kujihakiki na hata hawa waliofika hawakuwa na malalamiko dhidi ya mfuko, PSSSF tumekuwa tukulipa kwa wakati wateja wetu,"amesema 

 Amesema wateja wote waliofika wamekuwa wakipewa elimu ya namna ya kujihakiki kwa Simu zao kupitia  App ya PSSSF Kiganjani na kwamba elimu hiyo itaendelea kusambazwa ili kuwaondolea usumbufu wastaafu.

Aidha Katika kuadhimisha wiki ya wateja, wafanyakazi wa PSSSF Mkoa wa Arusha  waliofika kwaajili ya kupata huduma, ikiwemo waajiri   walipata fursa ya kula keki Maalum iliyotarishwa na mfuko huo pamoja na wafanyakazi kugawiwa miti.

Mtumishi wa mfuko wa PSSSF akimuhudumia mstaafu 


Awali akizungumza kwa niaba ya wastaafu waliohudhuria hafla hiyo fupi, mstaafu Yohana Sinda kutoka Mang'ola Barazanj Wilayani Karatu,  aliliomba shirika kuangalia uwezekano wa kuwasogezea huduma hizo Karibu na maeneo wanayoishi kwa kuwa baadhi yao wanatoka mbali na mji ambapo hutumia gharama kubwa za usafiri na malazi.


Chawe amesema miti hiyo imetolewa ikiwa ni mpango wa mfuko  kuunga mkono Serikali katika jitihada za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mstaafu wa Halmashauri ya Karatu aliyekuwa mtumishi Idara ya udereva, Pascal Gasino Manya akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mfuko huo Kanda ya Kaskazini Venos Koka ( aliyekaa kulia), 
Mkurugenzi wa Tehama wa mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSSSF, Gilbert Chewa pamoja na wastaafu waliofika katika ofisi za Kanda ya Kaskazini Jijini Arusha kwaajili ya kupata huduma wakishiriki zoezi la kukata keki ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya mteja

Mkurugenzi wa Tehama wa mfuko wa hifadhi ya Jamii PSSSF Gilbert Chewa akimlisha keki mmoja wa wastaafu waliofika katika ofisi za mfuko huo Kanda ya Kaskazini kwaajili ya kupata huduma 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post