SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI KWENYE KITUO CHA MAKAZI YA WAZEE NA WASIOJIWEZA KOLANDOTO

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga leo imetoa msaada wa nafaka na vitu mbalimbali ikiwemo  Sabuni, Mchele, Sukari pamoja na Mafuta katika kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto.

Akizungumza Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Madam Nabila Kisendi amesema kampeni hiyo imegusa na mahitaji ya wazee katika kituo hicho huku akiiomba jamii kuwa na majitolewa kwa watu wenye mahitaji.

Amesema kampeni hiyo itaendelea kuwa na majitoleo hasa kwa watu wenye mahitaji maalum  ambapo ametumia nafasi hiyo kuiomba jamii kupaza sauti kwa kutoa taarifa za ukatili unaoendelea kufanyika kwenye familia ili serikali iweze kuwachukua hatua za kisheria kwa watu watakaobainika kufanya vitendo hivyo.

Viongozi wengine  ni pamoja na katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya, Mwenyekiti idara ya michezo SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambaye ni polisi wa kata ya Ndala Afande Alkwin Willa pamoja na Mwenyekiti wa idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) wamewasihi wazee hao kuendelea kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na kuishi kama wanafamilia moja kwenye kituo hicho.

SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imetumia nafasi hiyo kuiomba jamii hasa familia zinazoishi na wazee kuendelea kuwapenda wazee, kuwafariji na kuhakikisha wanawapatia mahitaji yao ya msingi ikiwemo chakula pamoja na mavazi.

Kampeni  ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imetoa msaada wa Mchele, Mafuta ya kujipaka, Dawa ya meno, Sabuni za kipande pamoja na sabuni za unga, Sukari pamoja na Ubuyu kwa wazee katika kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto kilichopo Manispaa ya Shinyanga.

Katika kufanikisha msaada huo SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imeshirikiana na viongozi mbalimbali akiwemo Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale pamoja na Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Lydia Kwesigabo.

SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini inayotekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum ambayo  Wizara hiyo inaongozwa na Waziri Dkt. Dorothy Gwajima.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto Bwana Richard Maige pamoja na mwenyekiti wa wazee Kija Nyimbuge wameishukuru kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa msaada huo ambapo wamesema utawasaidia kupunguza changamoto zilizopo.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga na viongozi wengine wakiwasili katika kituo cha wazee na wasiojiweza Kolandoto leo Jumapili Oktoba 15,2023 kwa lengo la kutoa elimu ya ukatili pamoja na kukabidhi msaada wa nafaka na vitu mbalimbali kwenye kituo hicho.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga na viongozi wengine wakiwasili katika kituo cha wazee na wasiojiweza Kolandoto leo Jumapili Oktoba 15,2023 kwa lengo la kutoa elimu ya ukatili pamoja na kukabidhi msaada wa nafaka na vitu mbalimbali kwenye kituo hicho.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post