MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA MHE. MASUMBUKO ATEMBELEA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA KAMPASI YA SHINYANGA ASISITIZA UMUHIMU WA ELIMU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga  Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewataka wanafunzi katika chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kujielekeza kwenye elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.

Ameyasema hayo Alhamis Oktoba 26,2023 baada ya kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea chuo hicho ambapo amewasisitiza wanafunzi hao kutojihusisha na makundi ya wahalifu na badala yake wasome kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Mstahiki meya Mhe. Masumbuko amesema ni muhimu wanafunzi hao kujielekeza kwenye elimu kwa kuhakikisha wanasoma kwa bidii, na nidhamu ikiwa ni pamoja na kuzingaia sheria na taratibu zilizopo.

“Ni imani yangu kubwa sana kama mtazingatia haya ambayo mmeijia hapa chuoni naamini kabisa hamtatoka kama mlivyo mtatoka mmepata elimu ya kutosha ambayo inakufanya uende kutumika moja kwa moja kikubwa sana ni nidhamu kama huna nidhamu huwezi kuzingatia kile ambacho kimekufanya utoke huko unakoishi uje hapa kwa sababu ukikosa nidhamu utatengeneza mazingira ya nidhamu yako yakutokuwa na uoga kwa wale wanaokusimamia na hata huko nje mnakoishi mtaendelea kukutana na watu wenye tabia tofauti ebu mjielekeze tu ninyi kwamba mmekuja kutafuta elimu nasivinginevvyo”.amesema Mhe. Masumbuko

Mhe. Masumbuko ametumia nafasi hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha jambo hilo la kuleta chuo cha serikali za mitaa katika Mkoa wa Shinyanga.

Mstahiki meya huyo Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewahakikishia wanafunzi na walimu katika chuo hicho cha serikali za mitaa kuendelea kutoa ushirikiano wake katika shughuli mbalimbali za kuchochea maendeleo.

Kwa upande wake mkuu wa chuo Cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga  Dkt. Kasubi amewasihi wanafunzi hao kutokata tamaa na mwamba wanapaswa kuwa wavumilivu ili waweze kuhitimu salama.

Amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea kuzingatia yale yote wanayokubushwa na viongozi mbalimbali wa serikali ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema wataendelea kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ili waweze kufikia malengo yao.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga  Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiwasisitiza wanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao, baada ya kuwatembelea leo Alhamis Oktoba 26,2023.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga  Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiwasisitiza wanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao, baada ya kuwatembelea leo Alhamis Oktoba 26,2023.

Wanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga wakiwa katika hafla hiyo leo Alhamis Oktoba 26,2023.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post