Kaimu Kamishna Kuji aanza rasmi majukumu mapya TANAPA, awavalisha vyeo vipya makamishna wasaidizi

 Na Mwandishi Wetu, Arusha

Kaimu Kamishna wa Uhifadhi (TANAPA), Juma Kuji amewavisha vyeo vipya makamishna  wasaidizi waandamizi na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuwa mfano mzuri na kufuata taratibu za mfumo wa Jeshi la uhifadhi.


Zoezi la kuwavalisha vyeo Makamishna hao kutoka katika vitengo mbalimbali kwenye Shirika limefanyika leo Oktoba 10, 2023 katika Ofisi za Makao makuu ya Shirika jijini Arusha. 


Katika zoezi la kuwavalisha vyeo makamishna wasaidizi waandamizi Kaimu Kamishna, Kuji aliwataka Makamishna wote waliovaa vyeo hivyo kuwa viongozi wazuri katika maeneo wanayoenda kuyasimamia na kuwa mfano bora kwa askari na maafisa watakaowaongoza.

 


"Napenda mtambue kuwa cheo huwa kinakuja na majukumu, hivyo nawaelekeza mpitie majukumu yenu vyema ambayo mtapaswa kuyatekeleza. Na katika maeneo yenu ya kazi mnapaswa kuwa viongozi kwa kuonesha njia, hivyo nendeni mkawaunganishe maafisa na askari mtakaowasimamia ili kutimiza malengo ya Shirika tuliyojiwekea".


Aidha, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi ametoa wito kwa maafisa na askari wengine kutoa ushirikiano kwa viongozi hawa (makamishna wasaidizi waandamizi) waliovalishwa vyeo leo ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.


Kamishna Kuji alifunga tafrija hiyo kwa kuwataka viongozi wote wa Shirika kufanya kazi kwa uzalendo na weledi mkubwa ili kuliimarisha Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika kuongeza idadi ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi  ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post