JESHI LA POLISI SHINYANGA KUENDELEA NA UCHUNGUZI KATIKA TUKIO LA MTOTO WA MIAKA 12 MWANAFUNZI DARASA LA NNE NDEMBEZI KUJINYONGA

 

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwili wa mtoto aliyesadikiwa kujingonga hadi kufa mwenye umri wa miaka 12 anayetambulika kwa jina la Elisia Katondo mkazi wa mtaa wa Ndembezi Mwanoni katika Manispaa ya Shinyanga umesafirishwa leo kwenda Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza Baba mlezi wa marehemu huyo Bwana William Bayona amesema mwili huo umesafirishwa leo Jumanne Oktoba 17,2023kutoka Shinyanga kuelekea mkoani Kigoma nyumbani kwa wazazi wa marehemu,ambapo  baada ya kuwasili mkoani humo taratibu za mazishi zitafanyika.

Tukio la kujinyonga kwa Mtoto huyo limetokea Oktoba 15, Mwaka huu 2023 majira ya usiku.

Kwa upande wake Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Ndembezi Mwanoni Joice Tambwe amesema taarifa za tukio hilo alizipokea majira ya saa tatu usiku Oktoba 15,2023.

Aidha kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Elisia Katonda mwenye umri wa miaka 12, alikuwa anasoma darasa la nne shule ya msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

 

 

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post