Naibu Waziri Mkuu Biteko aagiza taasisi zote za umma zifanyiwe tathmini

 Na Ahmed Mahmoud


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko ameiagiza Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji Iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuzifanyia  tathimini taasisi zote za umma na Wizara bila ya uoga wala kumhofia yeyote katika ofisi hizo kwani ni za Watanzania wote.


Dkt. Dotto Biteko ametoa maelekezo hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu jijini Arusha wakati  kongamano la wiki ya kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathimini na Mafunzo inayofanyika kwa siku tatu katika kituo cha mikutano cha AICC jijini huo.


Amesema kwamba mjue serikali inatokana na wananchi, na wakati mwingine wananchi wanatufanyia tathmini sisi kuliko sisi tunavyojifanyia tathmini kama wananchi wanahitaji barabara kama wanahitaji,tathmini yao ya kwanza nikuona barabara ipo.


Alisema kwamba kama Kuna mipango tuiangalie,kama inatufikisha kwa haraka au inatukwamisha, hii ndio Kazi ya mkutano huu na Kazi yetu sisi kuangalia wapi tumekwama tuondoe changamoto hizo ili kuweza kutoa huduma stahiki.


"Ofisi ya Tathmini itakapokuja kwenu kutaka kujua utendaji wenu ni muhimu sana Tukaanza kubadilisha fikra na mitazamo yenu kwa kutoona taasisi ile unaofanyia Kazi ni Mali yako na mtu mwingine akitaka kuuliza jambo kanaibuka kahoja mnaniingilia,dhana hii inatuchelewesha sana"


Aliitaka Ofisi ya Tathmini kufanyakazi yake bila uoga Wala kumuogopa mtu ili kusaidia utendaji wa mipango ya serikali kuweza kwenda kwa weledi na ubora katika Lengo la kutoa huduma Bora kwa wananchi.


Awali akimkaribisha Dkt.Biteko Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama ameweka bayana mkakati wa kuimarisha kitengo cha ufutaliaji na Tathimini kwa kila taasisi za umma na ndio maana wameanzisha idara hizo kila wizara.


Kwa upande wake Mkuu Mkoa wa Arusha John Mongella ameeleza mafanikio ya kiuchumi yaliyofikiwa kutokana na ufanisi wa mipango ya serikali na kueleza suala la Ufuatiliaji na tathmini ni muhimu sana katika utendaji wa umma.


Katika kongamano hilo lenye washiriki zaidi ya 360 likilenga  kuleta Utayari, Uelewa na tija ya ufanisi katika Ufuatiliaji na utekelezaji wa mipango na Mikakati ya shuguli za serikali na ndipo Naibu Waziri Mkuu Dkt.Biteko anatoa maelekezo hayo


Kongamano hilo la siku tatu linawajumuisha  wataalamu na wadau kutoka taasisi za umma,makatibu  wakuu wa wizara, makatibu tawala wa mikoa, asasi za kiraia pamoja na wataalamu kutoka balozi za kigeni zilizopo nchini na wale wa Jumuiya za kikanda za SADC na EAC


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post