WAPIGA DEBE WAIFUNGA TIMU YA MNARA WA VODA 2-1 LIGI YA DR. SAMIA CUP SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Timu ya Wapiga debe imeibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja katika mchuano wao na timu ya Mnara wa voda kwenye ligi maalum ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA.

Mchezo huo umefanyika katika uwanja wa SHYCOM, na kwamba Mashindano hayo yameandaliwa na jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini kwa udhamini wa Taasisi ya Bega kwa Bega.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Jonathan Madete amewataja wafungaji katika mchezo huo.

“Wafungaji katika timu ya Wapiga debe ni Ramadhan Mbaga na Gerlad Devid lakini goli la timu ya Mnara wa voda limefungwa na Reonard John dakika za mwishoni”.amesema Mwenyekiti Madete

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Seleman Magubika ameendelea kuwapongeza waandaaji wa mashindano hayo, UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini kupitia udhamini wa Taasisi ya Bega kwa Bega.

 

 Awali wachezaji wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo wao leo Jumatano Agosti 30,2023.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post