Tanzania kushirikiana kimataifa kutunza misitu

1.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii CPA Mary Masanja akifungua Mkutano wa 13 wa CAFE Mapema Leo Jijini Arusha 

 Na Ahmed Mahmoud


TANZANIA Inakadiriwa kuwa na eneo la Misitu lenye takribani hekta 48.1 ambao huchangia katika uhifadhi wa bianuai makazi ya wanyama na uchavushaji wa mazao mbalimbali.

Aidha sehemu kubwa ya Misitu hiyo ni hekta Milion 25 ya mazao ya miombo ambayo huwezesha shughuli za ufugaji nyuki,utalii wa ikolojia na uwindaji wa kitalii na kuchangia asilimia 3-4 ya Pato la Taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii CPA Mary Masanja wakati akifungua Mkutano wa 13 wa Kimataifa CAFE unaojumusha mifuko 17 ya Maendeleo ya Misitu Kutoka nchi 20 za Afrika na mifuko minne Kutoka Amerika ya kusini na Carebean unaofanyika Kwa siku 5 Jijini Arusha.

Amesema  mifuko hiyo Inahitaji kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo kwenye Misitu ya Tao la mashariki Kwa kuhakikisha vipaumbele vinapewa nafasi kubwa ya kufikia malengo yaliokusudiwa.

"Tanzania itaendelea kushirikiana na mifuko mengine ya utunzaji wa mazingira Duniani na Afrika Kwa lengo la kusaidia utunzaji wa mazingira sanjari na Rasilimali za Misitu nchini mwetu hivyo Juhudi ziende sambamba kuongeza wigo na kupata uzoefu Kutoka Kwa wenzetu Ili kukuza Uchumi wa Jamii zetu".

A
2.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Deusdedit Bwoyo akiongea wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 13 wa CAFE Mapema Leo Jijini Arusha 
wali Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Misitu nchini EAMCEF Prof John Kessy Amesema Mfuko wa Tao la Mashariki ulioanzishwa na Serikali Kwa ajili ya shughuli za uhifadhi Maendeleo ya Jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi na Utafiti Kwa lengo la kuhakikisha kunakuwa na matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo kwenye Misitu ya Tao la mashariki.

Alisema Vipaumbele vyake vya Mfuko huo ni kuhifadhi Misitu katika milima ya Tao la Mashariki kukuza Uchumi wa Jamii zinazozunguka Misitu lakini pia kusaidia kuimarisha shughuli za Utafiti Ili kupata taarifa muhimu za kufanya maamuzi kama nchi.

Kwa Upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha Ramadhan Madeleka Amesema kwamba Mkoa huu umejaaliwa kuwa na utajiri wa Maliasili  na vivutio vya utalii vya asili na visivyo na asili ambavyo vinaambatana na Ngoma,ziwa Duluti Eyasi na mengineyo.

4.Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa 13 wakifuatilia Ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika Jijini Arusha.
Hata hivyo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Misitu SMZ Abbas Juma Mzee Amesema kwamba kama Zanzibar wamejipanga Kuangalia au kutunza Misitu yote ya juu na Ile ya kando ya bahari Kwa kuhakikisha misitu inatunzwa na kuhifadhiwa Kwa Faida kubwa ya vizazi vya sasa na vijacho.

Alisema Kwamba Mkutano huo ni fursa kubwa Kwa Zanzibar uwepo wa mifuko 19 kama ulivyo Mfuko wetu wa Maendeleo ya Misitu hili ni Jambo kubwa la kupata Uzoefu Pamoja na kujitangaza kujulikana Kwa lengo la kusaidia kuongeza wigo ikiwa sisi ni Mara ya kwanza kushiriki.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano huo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Deusdedit Bwoyo amesema kwamba Mkutano huo utasaidia kuongeza wigo wa Utafiti utunzaji wa Rasilimali za Misitu Pamoja na kujenga misingi ya utunzaji wa mazingira. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post