MHE. KATAMBI AZINDUA RASMI MALULA TV

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi, mgeni rasmi katikati akizindua rasmi taasisi ya habari za mtandaoni Malula TV usiku wa kuamkia leo siku ya Jumanne Julai 11,2023.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi amempongeza Daniesa Malula kwa kuanzisha Online TV taasisi ambayo itatoa ajira kwa vijana Nchini.

Mhe. Katambi ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Malula TV iliyofanyika katika ukumbi wa Malula Center uliopo kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo Jumanne Julai 11,2023 na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, taasisi binafsi pamoja, wadau mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mbunge Mhe. Katambi pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Malula TV kwa ubunifu na uthubutu wake wa kuambua kuanzisha taasisi ya habari ambayo itatoa fursa mbalimbali hasa kwa vijana Nchini.

Katambi amemsihi Mkurugenzi wa Malula TV, Bwana Daniesa Malula kutokukata tamaa huku akimsisitiza kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za Nchini.

Aidha Mhe. Katambi ameahidi kuendelea kushirikiana naye ambapo amesema atahakikisha changamoto zilizopo anazipunguza au kumaliza kabisa ndani ya muda mfupi ili kutekeleza majukumu yake bila vikwazo.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwaomba vijana wengine Nchini kuiga mfano huo wa Bwana Daniesa Malula kwa lengo la kuinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali ikiwemo Naibu meya wa Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ndala Mhe. Zamda Shabani pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Jonathan Madete wamempongeza Mkurugenzi wa Malula TV, Bwana Daniesa Malula kwa kufanikiwa kuanzisha taasisi ya habari ambayo itasabaza habari mitandaoni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Malula TV, Bwana Daniesa Malula amesema taasisi yake atahakikisha inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kanuni za tasnia ya habari Nchini.

TAZAMA PICHA ZOTE

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi awali akipokelewa na Mkurugenzi wa Malula Tv Bwana Daniesa Malula upande wa kulia.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post