UJENZI WA MADARAJA MAWILI KATA ZA KITANGILI, IBINZAMATA WAFIKIA ASILIMIA 90 YA UTEKELEZAJI, WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI.

Na Stela Shija Shinyanga

Ujenzi wa mradi wa madaraja mawili yanayounganisha Kata za Kitangili na Ibinzamata zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake.

Hayo yamebainishwa na Injinia anayesimamia ujenzi huo kutoka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, ambapo amesema ujenzi huo ulianza Mwezi Januari, 2023 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 24, 2023.

Mhandisi Yambi amesema mpaka kukamilika kwa mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi milioni 199 fedha ambazo zinatokana na mfuko wa jimbo zinazolenga kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkandarasi yupo katika hatua nzuri ambapo mpaka sasa ameshafikia asilimia 90 za utekelezaji, daraja la kwanza tumeshakamilisha ujenzi na tumesharuhusu wananchi kupita kwa muda wakati tunaendelea na ukamilishaji wa kazi zinazohusiana na barabara, maana mradi huu umegawanyika katika sehemu kuu mbili” amesema Mhandisi Yambi.

Tutachonga barabara na kuweka molamu karibu na daraja, ambapo kwa ujumla utekelezaji unaendelea vizuri, na kama nilivyosema hapo awali mradi huu unatekelezwa kwa fedha za miradi ya maendeleo ya jimbo. Na kwamba bajeti yake ilitengwa shilingi milioni 200 lakini kulingana na mkataba mpaka tunapotegemea kukamilisha mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi milioni 199, 968, 250/=” ameongeza Mhandisi Yambi.

Aidha, Mhandisi Yambi amesema asilimia 10 ilizobaki ni pamoja na kumwaga molamu karibu na eneo la daraja, kuweka alama za daraja, na kupaka rangi kwenye madaraja yaliyojengwa.

Ujenzi huu umetekelezwa kwa asilimia 90, hiyo asilimia 10 ilizobaki ni kazi ndogo ndogo za umaliziaji kuna kazi ya kuweka molamu karibu na eneo la madaraja, kuweka alama za madaraja ambapo tutaweka alama nne katika madaraja haya mawili, tutaweka alama inayohusiana na uzito wa magari mwisho kabisa tutapaka rangi kwenye madaraja na kazi itakuwa imekamilika kwa asilimia 100” amesema Mhandisi Yambi

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na kuipongeza serikali kwa uboreshaji wa miundombinu hiyo, wamesema madaraja hayo yatarahisisha wamasiliano kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ikilinganishwa na hapo awali ambapo walikuwa wakipata usumbufu hasa wakati wa masika.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post