WAZAZI WATAKIWA KUZINGATIA MALEZI KWA WATOTONa Elias Gamaya Shinyanga 
Jumuiya wa wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Shinyanga Mjini Mkoani Shinyanga imewaomba wazazi kuzingatia malezi wa watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia mienendo yao haswa nyakati hizi Ulimwengu unakabiliwa na Ongezeko la Vitendo vya Ushoga, Ubakaji, Ulawiti na Usanganaji. 

Hayo yamezungumzwa na Wazazi wa Jumuia hiyo wakati walipokutana na wazazi na wawakilishi wa Jumuiya hiyo kata ya Lubaga halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga. 

Akizungumza katibu wa jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Yotham kibabi Amebainisha aina ya ukatili unaoendelea ikiwemo Ukatil wa kingono, ukatili wa kisaikolojia, ukatili wa kumwili pia ukatili wa kiuchumi ambapo kawasihi wazazi kuzingatia malezi ya watoto ili kujenga taifa lililo bora Sambamba na hayo Katibu wa jumuiya hiyoDoris Yotham amewaasa wazazi kuepukana na Mila potofu ikiwemo ukeketaji kwa watoto.

 "Mungu ametupa viungo vyote na kila kiungo mwilini kinakazi yake kwahiyo tusidanganywe na hao Ngariba, tunapokiondoa tunakaribisha Magonjwa mengine na kupelekea vifo kwa watoto wetu" Amesema Doris Yotham Katibu Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga.

" Mauaji mengine yanasababishwa na vitendo vya Ukatili, unakuta baba zima linamuingilia mtoto wake wa kuzaa, mtoto anakua hajakomaa, au mama unakuta anamwambia mwanae uniletee chips wakati unajia Mwanao hana ajira unategemea nini hapo mtoto ni kwenda kujiuza tu" Amesema Doris Yotham Katibu wa jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga.

Nao baadhi ya wazazi wameeleza sababu za ongeko la wimbi la ushoga, Ulawiti, Usanganaji na ubakaji. 

"Watu sikuhizi hatumjui kabisa Mungu hatufuati mafundisho yaani tunajiita tunasali kumbe ni Wapagani tuliochangamka, kama tungekua tunafuata mafundisho huwezi kufanya usagaji, ushoga, urawiti wala Ubakaji" Amesema Grace mpemba. Mkazi Lubaga

"Sisi wazazi tumewaacha watoto wanazurura mpaka usiku sana watoto wengine wanalala kwenye mitalo kwa sababu wazazi tumewatelekeza hali inayowapelekea kujiingiza kwenye Magurupu mabaya" Amesema Mathias Sheka Mkazi wa Lubaga 

Nae mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Fue Mrindiko wilaya ya shinyanga amewasihi viongozi wa Kata kushirikiana na wananchi ili kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.

"Viongozi tushikane tusigongane gongane wala kusiwepo na wasaliti, tupendane tuwe kitu kimoja ili kuwaletea maendeleo wananchi wetu" Amesema Fue Mrindiko Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini.

 Sambamba na hayo jumuiya hiyo imetembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu Shinyanga Sotiety for Orphans kilichopo Bushushu na kutoa misaada mbalimbali kwenye kituo hucho ambapo Mkurugenzi wa kituo hicho Ayam Ally Said ameishukuru jumuiya ya wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwaomba watanzania wote kuendelea kuwaona na kuwasaidia watoto hao kwani wanahitaji Ukaribu wa wazazi.


"Niwashukuru sana wazazi hawa kujakutuona hapa kituoni kwan watoto hawa niwaombe saba wananchi tuendelee kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu" amesema Ayam Ally Said mkurugenzi wa Shinyanga Society for Orphans

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post