SHIRIKA LA HAKI YANGU FOUNDATION LAZINDULIWA RASMI, MKURUGENZI MHE. SALOME MAKAMBA ATAJA MALENGO

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.

Shirika jipya lisilo la kiserikali la HAKI YANGU FOUNDATION limezinduliwa rasmi leo katika ukumbi wa African Dreams Mkoani Dodoma na   litajikita katika miradi ya kutetea na kusaidia wanawake na watoto wenye uhitaji Nchini hasa katika Mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha miaka mitano.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi muasisi na mkurugenzi wa shirika hilo ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA, Bi. Salome Makamba ametumia fursa hiyo kubainisha malengo ya shirika kuwa ni kusaidia jamii katika masuala ya    kisheria, kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya Haki Yangu amesema Mkoa wa Shinyangani moja ya eneo litakalofikiwa sana huku baadhi wa wadau waliohudhuria uzinduzi huo wakipongeza juhudi hizo.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya shirika la Haki Yangu Bwana Richard Haule amesema Mkoa wa Shinyanga ni moja ya eneo litakalofikiwa na ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo  kutoa ushirikiano pindi shirika hilo litakapowafikia.

Uzinduzi wa Shirika la Haki Yangu umehudhuriwa na viongozi wa serikali ,vyama vya siasa na wadau mbalimbali huku Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Felista Njau pamoja na Mbunge wa CCM jimbo la Kasulu Vijijini Mhe. Vuma Agustine wamepongeza upunifu na hatua aliyoifanya Mhe. Salome Makamba katika kusaidia na kutetea haki za wanawake na watoto ili kupunguza au kumaliza kabisa ukatili uliopo katika jamii.

Muasisi na mkurugenzi wa shirika la Haki Yangu Fondation ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA, Bi. Salome Makamba akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa shirika hilo.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Grace Victor Tendege akizungumza kwenye uzinduzi wa shirika la Haki Yangu uliofanyika Mkoani Dodoma.Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Grace Victor Tendege akizungumza kwenye uzinduzi wa shirika la Haki Yangu uliofanyika Mkoani Dodoma.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Felista Njau akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa shirika la Haki Yangu Foundation uliofanyika Mkoani Dodoma.

Hafla ya uzinduzi wa shirika la Haki Yangu Foundation ikiendelea katika ukumbi wa African Dreams Mkoani Dodoma.

Muasisi na mkurugenzi wa shirika la Haki Yangu Fondation ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA, Bi. Salome Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waliohudhuriwa uzinduzi wa shirika hilo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post