Mtatiro: Wazazi,walezi chungeni watoto chini ya miaka 8

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro
 
Joyce Joliga,Tunduru

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwa mstari mbele katika malezi ya watoto wenye umri chini ya miaka 8 pamoja na vijana kulingana maadili ya Mtanzania.


Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma.


Mtariro ameongeza kuwa Taifa linapaswa kusonga mbele likiwa salama kwa kuwalinda watoto na vijana wasiweze kuiga tabia za mataifa yaliyoporomoka kimaadili.


"Wazazi wakiacha kutekeleza wajibu wao kwa watoto hatutaliokoa Taifa, na kama Yesu Kristo alibeba msalaba wake mpaka mwisho kumkomboa mwanadamu iweje wazazi washindwe kusimama kidete kwa ajili ya malezi bora ya watoto". amesema Mtatiro


Pamoja na mambo mengine amewakumbusha Wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujiwekea akiba ya chakula, badala kukiuza kabla ya msimu na kusababisha migogoro ya kifamilia.


Nao baadhi ya waumini akiwemo Samwel Mzava ameshukuru viongozi kwa kuendelea kukemea mmonyoko wa maadili hasa kwa watoto wadogo. 


Naye Chritina Mahundi amewataka wazazi na walezi kuzingatia maelekezo yanayotolewa na viongozi pamoja na kuwa walinzi namba moja wa Watoto.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post