KATA YA NDALA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DIWANI ZAMDA ATOA MSAADA KWA WAZEE WASIOJIWEZA" DC SAMIZI AKEMEA WIMBI LA ULAWITI NA UBAKAJI

Na Mwandishi wetu 

Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga imeazimisha sherehe za siku ya wanawake kwenye kata huku ikifanyika na kutoa msaada kwa wazee wasiojiweza kwenye kata hiyo.

 Hafla hiyo imefanyika tarehe 01/04/2023 katika viwanja vya soko la Ndala lililopo Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine wamepanda miti 250.

Akiongea mbele ya wananchi hao Diwani wa kata hiyo Mhe. Zamda Shaban amewahakikishia wakazi wa  kata hiyo kuwa sherehe hizo zitakuwa zinafanyika kila Mwaka ili kuendeleza umoja, mshikamano na upendo.

" Ndugu zangu Wana Ndala leo ni siku maalumu, tuliyoitenga  kwa ajili ya kuzungumza,kucheua na kupeana zawadi kidogo, hivyo tutakua tunafanya kila mwaka ili kujenga umoja kwenye kata yetu"

Aidha akitoa taarifa kwa mgeni rasmi ambae alikua Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Johari Samizi diwani huyo alisema

" _Mheshimiwa hapa tuna soko letu la kata ya Ndala, Hili soko Lina zaidi ya miaka 20 halifanyi kazi,wamama walikuja hapa wakawekeza,wakajenga vizimba, na vibanda lakini halijafanya kazi, hivyo tunaomba ulifatilie ili tupate ufumbuzi"_ alisema Diwani Zamda

 Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga  Mhe. Johari Samizi kabla ya shughuli hiyo alipata nafasi ya kupanda mti wa mwembe eneo ofisi ya kata ya Ndala.

 DC Samizi pamoja na mambo mengine wakati akizungumza na wananchi amekemea  vikali suala la ulawiti na kuwataka wazazi kulea watoto katika maandili mema ili kuandaa Taifa bora.

"Ndugu zangu, wazazi wenzangu tuna jukumu kubwa Sana la kuilinda jamii, na ulinzi wa mtoto unaanza nawewe mzazi, hivyo niwaoambe wazazi wote tujitahidi kuwalinda watoto, tufatilie shule wanazosoma, tufatilie mienendo yao pia tusiruhusu watoto kuangalia katuni zisizofaa, na zisizo na maadili kwenye jamii yetu".amesema DC Samizi

 Sherehe hizo zilipambwa na utolewaji wa zawadi na misaada mbali mbali  kwa wazee 110 kutoka kata ya Ndala yote na zawadi hizo zlikua ni unga kilo tano kwa kila mzee,sukari,sabuni na mche mmoja wa mti wa mwembe

 Akizungumza kwa niaba  ya wazee wote waliopata msaada huo Mama Juma mkazi wa mtaa wa Mwabundu, alisema

"Namshukuru Sana Diwani Zamda kwa kutukumbuka sisi wazee wa Ndala, haswa wamama hatuna chakumlipa na tunaahidi kumuombea kwa Mungu azidi kumbariki maradufu,na alipotoa azidi kuongezewa, alisema mama Juma aliyepata msaada huo"

Kauli mbio ya Mwaka huu inasema “NDALA BILA UDUMAVU WA WATOTO NA CHAKULA SHULENI INAWEZEKANA”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post