JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LAPONGEZWA KAMANDA MAGOMI TULIIMARISHA DORIA SIKUKUU YA PASAKA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa kufanya doria katika maeneo mbalimbali hali iliyosaidia wananchi kusherehekea sikukuu ya Pasaka katika mazingira ya Amani ya utulivu.

Kwa nyakati tofauti Misalaba Blog imezungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga ambao wamelipongeza jeshi la Polisi kuwajibikia vyema jukumu la ulinza na usalama wa raia na mali zao katika kipindi chote cha sikukuu ya Pasaka

Wameeleza kuwa licha cha kuwepo kwa changamoto kadhaa zilizotokana na ukiukwaji wa matumizi sahihi ya vyombo vya usafiri lakini jeshi la polisi liliimarisha ulinzi kupitia doria zake mbalimbali.

Mwenyeviti wa wenyeviti wa serikali za mitaa katika Manispaa ya Shinyanga Bwana Nassor Mokhe Worioba naye  ametumia nafasi hiyo kulipongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao huku akiwakumbusha watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Akizungumza na Misalaba Blog  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema hali ya usalama ni shwari na kwamba jeshi hili limeendelea kuimarisha doria katika maeneo mbalimbali ya wananchi.

ACP Magomi amewashukuru wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kuzingatia na kufuata sheria, kanuni  na taratibu zilizopo katika kuimarisha usalama.

Mwenyeviti wa wenyeviti wa serikali za mitaa katika Manispaa ya Shinyanga Bwana Nassor Mokhe Worioba aliyevaa kibarakashia upande wa kulia akiwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga ambao wamelipongeza jeshi la Polisi kwa kuimarisha ulinzi na usalama kipindi chote cha sikukuu ya Pasaka

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post