![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Arusha akiwa na watendaji wa Taasisi za Serikali zinazohusika na uwekezaji katika Mkoa wa Arusha |
SIASA mbaya katika Jiji la Arusha zimeelezwa kukwamisha wawekezaji kuwekeza katika Jiji hilo na hivyo kuikosesha Serikali mapato mengi ambayo yangetokana na fursa hizo.
Hayo yameelezwa Leo Machi 23, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa alipokuwa akifungua Kikao kilichokutanisha idara na taasisi za Serikali Mkoa wa Arusha ambazo zimekuwa zikihusika moja kwa moja na uwekezaji.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa akifungua Kikao maalum Cha watendaji wa Serikali wanahohusika na uwekezaji ndani ya Jiji la Arusha |
Amewataka watendaji wa Taasisi za Serikali zinazohusika moja kwa moja na uwekezaji kutojiingiza kwenye siasa hizo mbaya na badala yake wamsaidie Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuongeza uwekezaji na kuinua uchumi wa nchi.
Aidha ameziagiza taasisi hizo kuandaa kitabu kimoja kitakachokuwa kimeainisha maeneo ya uwekezaji, na namna mwekezaji ataweza kufaidika na maeneo hayo ili kuvutia wawekezaji wengi kuja Jijini Arusha.
![]() |
Meneja wa kituo Cha uwekezaji Kanda ya Kaskazini Daudi Riganda akizungumza katika kikao hicho |
Amesema katika sheria hiyo mpya, kituo Cha uwekezaji kimefanyia mabadiliko sheria nyingi ikiwemo ya mitaji ya uwekezaji kwa wazawa na wageni lakini pia kuongeza muda wa kuanza kulipia kodi, pamoja na idadi ya wafanyakazi wanaotakiwa kuwepo katika eneo linaloanza uwekezaji.
Aidha Riganda amesema kituo cha uwekezaji kimeanzisha utaratibu wa kutoa huduma za uwekezaji katika kituo kimoja ( One stop facilitation center) ambapo taasisi zote za Serikali zinazohusika na nyaraka za uwekezaji nchini zitakuwa katika kituo hicho.
" Ukiachilia mbali utaratibu mpya wa kutoa huduma za uwekezaji katika eneo Moja kwa taasisi zote husika, Serikali iko kwenye hatua za kukamilisha dirisha la utoaji huduma kwa njia za kielekroniki, na taasisi 12 tayari zimeunganishwa lengo likiwa ni kushughulikia utoaji vibali, leseni kwa urahisi na uharaka, ndani ya siku3," amesema Riganda.
![]() |
Washiriki wakifuatilia |
Katibu Mtendaji wa Chama Cha waendesha utalii Tanzania ( TATO), Cyrill Ako amesema wawekezaji katika sekta ya utalii wamekuwa wakiomba kufanyiwa mabadiliko kwa sheria ya District Service Levy, ambayo imekuwa kero kubwa kwao baada ya kila Halmashauri kufanyia usumbufu kampuni za utalii zikitaka kupewa Kodi hiyo.
" Sisi kama TATO tunaomba hii sheria ifanyiwe mabadiliko, gari ikitoa na mgeni kuanzia KIA inapita Wilaya nyingi sana hapa katikati, kila Halmashauri inakuja ofisini kudai Kodi Ile Ile, kwanini isiwekwe sehemu Moja tukajua tunatakiwa tulipie kiasi Fulani badala ya usumbufu kwa kila mtu?," alihoji Akko.
![]() |
Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa |