HALI NI MBAYA MASHOGA SHINYANGA DC SAMIZI, VIONGOZI WACHUKIZWA NA MAMBO HAYA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameitaka jamii, viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali kushirikiana ili kutokomeza mmomonyoko wa maadili kama ukatili, mapenzi na ndoa za jinsia moja.

Ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Mwaka 2022/2023 kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022 kwenye mkutano ambao umefayika katika ukumbi wa ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

  DC Samizi amesema ushirikiano wa kupambana dhidi ya mmomomnyoko wa maadili utasaidia kuendelea kukuza na kulinda mila, desturi na maadili mema ya Kitanzania.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya   amesema serikali itaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inachukua hatua kali kwa taasisi zitakazo bainika kujihusisha na uhamasishaji mapenzi na ndoa za jinsia moja katika Wilaya ya Shinyanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Anord Makombe amesema serikali iendelee kuchukua hatua kali kwa wanaobainika kufanya mambo hayo katika jamii.

Naye katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Bwana Ally Ally amewasihi wananchi kuungana na serikali kupinga vitendo hivyo ili kuimarisha usalama wa Taifa.

Wakati huo huo leo Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wamepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya Mwaka 2022/2023 katika kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022.


















This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post