BADO SIKU 2 UHAKIKI WA LESENI KWA HIARI, ASP KAIGWA AWAPA TAHADHARI MADEREVA WILAYA YA SHINYANGA

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Polisi kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga ASP Dezidery Kaigwa amewataka madereza wanaomiliki leseni za kuendesha abiria pamoja na mizigo kufika kituo cha Polisi makao makuu kwa ajili ya zoezi la uhakiki Wa leseni zao.

ASP Kaigwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Misalaba Blog ofisini kwake ilipomtembelea ili kufahamu mwenendo mzima wa zoezi la kuhakiki leseni za madereva linavyoendelea.

 Amesema kuwa zoezi la uhakiki wa leseni kwa hiyari litafanyika hadi Machi 31 Mwaka huu 2023 na baada ya muda huo itaanza operesheni ya ukaguzi.

Wakati huo huo ASP Kaigwa amebainisha kuwa lengo la uhakiki huo wa leseni ni kubaini madereva ambao wanaendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na sifa hitajika kisheria.

Ukaguzi huo wa leseni za madereva wa vyombo vya moto kwa hiari umeanza rasmi tarehe 3 mwezi Machi 2023 na utafikia tamati tarehe 31 mwezi huu.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post