Nabii Geodevie akamilisha ahadi yake

 MILIONI 100 ZATOLEWA KWA WAFANYABIASHARA NA NABII MKUU DKT GEORDAVIE ARUSHA.


Na Jane Edward,Arusha

Wafanyabiashara katika soko la samunge jijini Arusha wameshukuru kwa ahadi ya kupatiwa fedha shilingi Milioni 100 zitakazo tumika kwaajili ya kukuza mitaji yao.


Nabii Mkuu Dkt GeorDavie alitoa ahadi hiyo januari 23 mwaka huu katika soko hilo, baada ya kupokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara hao juu ya uhitaji kutokana na kuunguliwa kwa soko hilo miaka minne iliyopita na kupoteza Mali zao .


Akikabidhi mfano wa hundi hiyo kwa mwenyekiti wa wafanyabiashara kwa niaba ya Nabii mkuu GeorDavie,katika hafla iliyofanyika katika soko hilo,

 msaidizi wa Nabii, Balozi ,Sekela Ntondolo aliwataka wafanyabiashara hao kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.


"Leo nimekuja kukabidhi fedha hizo sh,milioni 100 alizoahidi nabii mkuu na nitakabidhi na nakala ya malipo ya benki inayoonesha fedha hizo tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti ya wafanyabiashara wa soko la Samunge"


Awali mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo Njola Miraji, alimshukuru nabii mkuu kwa kutimiza ahadi yake akidai kuwa wapo mabilionea waliotokana na madini ya Tanzanite lakini wameshindwa kusaidia jamii yenye uhitaji .


Alisema katika fedha hizo wameorodhesha majina ya wafanyabiashara 1261watakaonufaika na fedha hizo na tayari majina hayo ameyakabidhi kwa nabii mkuu kama alivyoelekeza wakati akiahidi fedha hizo . Naye mkuu wa soko hilo,Restituta Nyoni aliwataka wafanyabiashara watakaonufaika na fedha hizo kuzielekeza kwenye biashara husika na kuepuka kuzipeleka kwenye mambo yasiofaa ikiwemo kwenye vikoba.


"Endapo utapokea hizo fedha nenda kafanye biashara usiende kunywea pombe au kuingiza kwenye vikoba"


Baadhi ya wafanyabiashara hao wakiwemo wadau wa maendeleo walimshukuru nabii Mkuu Geordavie kwa moyo huo na ukarimu wake na kuwataka wafanyabiashara na watumishi wengine wa mungu kuiga mfano huo ili kuisaidia jamii yenye uhitaji.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post