Kiwanda cha mataruma ya reli ya kisasa kuokoa fedha za kigeni

 Na Ahmed Mahmoud

Kiwanda cha utengenezaji mataruma ya Reli ya kisasa SGR Lot 5 Mwanza Isaka kinatarajiwa kuokoa fedha za kigeni na kupunguza kuagiza nje ya nchi vifaa hivyo na hivyo kuongeza mzunguko wa kiuchumi.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari waliotembelea Mradi huo eneo la Seke Kata malampaka Mkoa wa Simiyu Mhandisi wa  Mradi huo Daniel Nyanda Amesema kiwanda hicho ni mkombozi wa kiuchumi Kwani kimeweza kuajiri wafanyakazi 139.

Alisema kwamba Pamoja na kuajiri wafanyakazi hao ambao wote ni Watanzania pia kitazalisha matarama yote katika Mradi huo na kina uwezo wa kuzalisha mataruma 500,000 ambayo yatatumika katika eneo la Isaka hadi Mwanza Lot 5 

"Hadi Sasa tumeshaanza uzalishaji huo pia majaribio Kwa Kipande Cha Awali Cha Seke Kwa mita 100 hichi kiwanda kitasaidia Sana matengeneze ya mataruma haya na uzoefu Kwa vijana wa kitanzania"

Kwa Upande wake Meneja mradi huo Kutoka Shirika la reli TRC Mhandisi Christopher Kalist anasema kwamba mradi huo hadi Sasa umefikia asilimia 19 na Tuta asilimia 46 na wapo ndani ya muda ambapo Kazi ya ujenzi wa madaraja unaendelea Kwa Kasi kubwa.

Amesema kwamba hadi kufikia Sasa kama hakutakuwa na changamoto ya hali ya hewa ifikapo mwezi wa Tatu wamejiwekea malengo ya kufikia asilimia zaidi ya 50 kukamisha mradi huo.

"Utaratibu tuliojiwekea ni kufikia asilimia zaidi ya 50 Kwa Kasi hii anayoendanayo mkandarasi ifikapo mwezi 3 mwakani iwapo hali ya hewa itakaa sawa Kwani maeneo mengi aliyohitaji mkandarasi tumepatia km 256 ya ardhi yote imebakia maeneo machache Sana ambayo tunaendelea na mazungumzo na wamiliki Ili tufanye uthamini"

Nae Mhandisi Marry Kileleu anayesimamia mazingira katika Mradi huo anaeleza kwamba wao wamejipanga kuhakikisha mkandarasi anazingatia suala Zima la sheria za mazingira yote anayofanyia Kazi Kwa lengo la kutunza mazingira yeto inamopita mradi huu.

Kuhusu suala la uzingatiaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira,alisema kuwa wamekuwa wakimshauri Mkandarasi kufuata Sheria za Mazingira ili kutimiza matakwa ya Serikali.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post