Wadau wa utalii waandaa Marathoni kutangaza Hifadhi ya Arusha

Lomayani Komolo, muandaaji wa mbio hizo

Katika huhimiza utalii wa ndani nchini Tanzania, Lomayan Komolo Simel kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa wanyamapori na utalii wameamua kutumia njia  ya michezo  kutangaza hifadhi ya Taifa ya Arusha iliyopo karibu na mji wa Arusha pamoja na kusapoti jitihada za serikali ya kuzitangaza hifadhi zetu za taifa.


Akizungumza na waandishi wa habari mwanzilishi mkuu wa mbio hizo na mratibu mkuu mtendaji wa Arusha Park wildlife Marathon  Lomayan Komolo amesema kuwa wameandaa riadha  ambayo ni tofauti na ya kipekee Tanzania kwakuwa kwa asilimia mia moja mbio zote zitakuwa ndani ya hifadhi na sio nje ya hifadhi.


Amesema kuwa marathoni  hiyo itakuwa na mbio aina tatu ambapo mbio ya kwanza itakuwa kilomita 5 Fun run, 10km na Half marathon 21km,pia mbio hizi zitakuwa zinaanza mahali moja na kumalizikia mahali moja ni one way run, yaani unamalizia huko huko bila Kirundi njuma kama mbio nyingi tulizo zoea, pia hifadhi ina mathari mazuri pamoja na wanyama ambako wakimbiaji watakuwa na fursa ya kukimbia pembezoni mwa wanyama kwahiyo watawaona wanyamapori


Amesema marathon hiyo itakuwa na Ghaarama kidogo ambayo ndio kiingilio na marathoni hiyo usalama utakuwa mkubwa sana hivyo anawatoa watu wote hofu  Kwa asilimia mia Moja usalama upo.


Amesema lengo la mbio hizo ni kutangaza hifadhi ya Arusha kwani ni hifadhi ambayo watu wengi waliopo Moshi na Arusha pamoja na mikoa jirani hawaijui lakini lengo lingine ni kuchangia  fedha Kwa ajili ya kungoa magugu vamizi ambayo ni hatarishi Kwa wanyamapori ndani ya hifadhi ya Arusha. 


Amesema kuwa marathoni hiyo pia ni fursa ya  kutangaza huduma mbali mbali zinazo tolewa na wawezeshaji wa mbio hizi za Arusha Park Marathon, kukuza vipaji kwa wakimbiaji chipukizi vilevile jamii pia itajifunza mambo mengi ya uhifadhi na utalii.


Amesema kuwa gharama zinatofautiana Kwa jumuiya afrika mashariki 35,000/= Kwa ajili ya kiingilio,wageni wa nje wanafanya kazi Tanzania gharama ni 120,000/= na watalii wa nje ni gharama ni 190,000


Amesema kuwa Kwa wakimbiaji wote watapatiwa medali, tishert na riboni mkononi,vikombe Kwa washindi kuanzia namba 4 Hadi 10 na pesa kias kwa washidi wa 1-3 ,vile vile kutakuwa na huduma za majii, matunda na glucose ili kuwapatia nguvu wakimbiaji njiani.


Amesema kuwa Kwa wale watakojisajili Kama timu au clubs mkoani Arusha na Moshi kufikia kiwango cha watu 30 watapatiwa usafiri Bure.


Amesema kuwa Kwa wale ambao wana watoto wadogo watachangua gharama kidogo na pia Kwa wale watakotamani kulala vile watachangia kidogo


Hata hivyo katika marathon hiyo zaidi ya washiriki 400 wanatarajiwa kushiriki ambapo pia Kwa anayehitaji tiketi zipo sehemu zifuatavyoo  kwa mini Arusha fika maeneo yafuatayo office ya TTB clock tower,Kipong mkabala na polisi na Jengo la Condo kaloleni ground floor chumba number 5 na Kwa mji wa Moshi unaweza kufika chuo cha wanyamapori Mweka na Kibo Cleaning services (Kwenye tawi la Viva Yanga Kilimanjaro) opposite na coffee Curing


Sanjari na hayo Mhazilishi huyo amesema zoezi Hilo litakuwa endelevu na amewataka wanariadha kote nchini kujitokeza ipasavyo hiyo tarehe 4/12/2022 kukimbia hii mbio ya kipekee kabisa Tanzania.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post