vodacom kugawa simu milioni 1.5 kwa vikundi vya polisi shirikishi

Na Magesa Magesa , Arusha

KAMPUNI ya simu ya Vodacom Kanda ya Kaskazini inatarajia kugawa simu milioni 1.5 kwa vikundi vya polisi shirikishi lengo likiwa ni kusaidia kurahisisha mawasiliano kati ya vikundi hivyo na Jamii.

Meneja wa Vodacom,kanda ya Kaskazini George Venanty aliayasema hayo jana alipokuwa akigawa simu kwa baadhi ya vikundi hivyo katika mitaa 33 jijini hapa na kusema kuwa zoezi hilo litakuwa likifanywa kwa awamu lengo likiwa ni kuvifikia vikundi vyote katika kanda ya kaskazini. 

 “Sisi Vodacom tunaamini katika amani utulivu na usalama wa jamii na ndio maana tumeamua kutoa simu hizo ili kurahisisha mawasiliano pindi jamii inapoona kunataka kutokea tukio la uhalifu kuweza kuwasiliana moja kwa moja kupitia simu hizo ambazo zina namba maalumu” alisema.

 Venanty Aliongeza kuwa waliamua kutoa simu hizo sio tu kwa kurahisisha mawasiliano bali bia ni kurudisha sehemu ya faida wanayoipata katika kusaidia jamii na kuwataka wale wote watakaokabidhiwa simu hizo kuhakikisha kuwa wanazitunza na kuzitumia kwa lengo lililokusudiwa.

Alisema kuwa simu hizo zitakuwa na namba maalumu ambazo zitakuwa zikiratibiwa na jeshi la polisi ambapo endapo mwananchi atahisi kunataka kutokea au kumetokea tukio la uvunjifu wa amani atatakiwa kuwasiliana moja kwa moja kupitia simu hizo. 


 Kwa upande wake kaimu Kamanda wa polisi Mkoani hapa,Mary Kipesha aliipongeza Vodacom kwa msaada wao huo na kusema kuwa umekuja wakati muafaka kwani utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na uhalifu mkoani hapa. 


 Aliongeza kuwa usalama wa raia na mali zake ndio kila kitu na ndio maana jeshi la polisi liliamua kuweka wakaguzi wa polisi kila Kata ili washirikiane na vikundi hivyo vya polisi shirikishi katika kupamabana na kukabiliana na uhalifu. 


 “Sisi polisi lengo letu ni kuhakikisha tuna pata taarifa za uhalifu kabla uhalifu huo haujatokea ili tuweze kuwabaini wahalifu na kukabiliana nao mara moja na ndio maana tuliamua kuunda vikundi hivi na tayari vimeonyesha kuleta tija katika jamii inayowazunguka” alisema.


Kipesha Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Edith Swebe aliitaka jamii kuhacha mara moja kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua kali yeyote Yule atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo. 


 Alisema kuwa jukumu la kulinda usalama sio la jeshi la polisi pekee bali ni la kila mtu hivyo wakati umefika kwa kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake kwani lengo likiwa ni kukabiliana na uhalifu kwani Arusha bila uhalifu inawezekana.
Baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi na vikundi vya polisi
shirikishi wakifuatilia zoezi la ugawaji wa simu zilizotolewa na
kampuni ya mawasiliano ya vodacom ili kurahisisha mawasiliano kati ya
vikundi hivyo na jamii
wafanyakazi wa vodacom wakipata maelezo kutoka kwa mmoja maofisa wa
kampuni hyonamna ya kuzisajili kadi maalumu za simu zilizotolewa na
kamuni hiyo kwa vikundi vya polisi shirikishi(picha zote na Magesa
Magesa

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post