Afariki kwa kujinyonga

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Juma Hamis mkazi wa mtaa wa Iwelyangula kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga amekutwa amefariki Dunia kwa kujinyonga na kamba kwenye mti.

Tukio hilo limetokea leo Septemba 12,Mwaka huu 2022, majira ya saa saba mchana ambapo marehemu Juma Hamis amekutwa amejinyonga kwenye Bustani ya matunda mtaa wa Sanjo Kata ya Chamaguha iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

Misalaba Blog imezungumza na Mwenyekiti wa mtaa wa Iwelyangula Bwana Robert Mnyeleshi ambaye ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa mfanyakazi wake akitokea Mkoa wa Kigoma na kwamba, baada ya kumaliza kucheza mpila siku ya jana jioni hakurudi Nyumbani.

“Jana alikuwepo kwenye saa kumi na mbali alikuwa anacheza mpila na vijana wenzake lakini baada ya kumaliza kucheza mpila hakurudi nyumbani tena tukaanza kumtafuta usiku huo hatukuweza kumpata asubuhi tumeamkia kumtafuta ilipofika  muda wa saa saba mchana wakaja vijana wawili walipita huko kwenye bustani wakaona mtu ameniny’inia waliponipa taarifaa nikaenda kujiridhisha nikaona ni kweli ikabidi nipige siku polisi”

“Kabila lake ni Muha mzaliwa wa Kigoma alikuja kwangu anatafuta kazi nikampa kazi ya  kuchunga Ng’omba”. amesema Mwenyekiti Mnyeleshi

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amethibitisha kupokea taarifa za kijana huyo na kwamba jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

“Nathibitisha kweli kupata taarifa hizo na jeshi la polisi limeshafika pale kwa ajili ya kuchukua mwili lakini hajaacha ujumbe wowote bado tupo kwenye upelelezi ili kubaini chanzo”.amesema Kamanda MagomiThis is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post