Wasanii Shinyanga waunga mkono sensa

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkurugenzi wa CM Entertainment, Clouds Charles Malunde ameanzisha tamasha na baadhi ya wasanii wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuiunga mkono serikali kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika  Mwaka huu 2022.


Tamasha hilo ambalo limeanza leo Ijumaa Agosti 20,Mwaka huu 2022 katika uwanja wa Risasi uliopo karibu na Mazingira center Manispaa ya Shinyanga ambapo wasanii kutoka katika makundi mbalimbali ya aina ya mziki wameimba kwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi.


Akizungumza Mkurugenzi huyo wa CM Entertainment ambaye ndiye mdhamini wa tamasha hilo ameeleza kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi linahitaji nguvu ya pamoja ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.


Amesema ameamua kuanzisha tamasha hilo kwa kuwashirikisha wasanii kutumia kalama zao za uimbaji kwa lengo la kufikisha ujumbe wa sensa  kwenye jamii ili iweze kujitokeza kwa wingi.


''Nimeandaa hili tamasha nashirikiana na wasanii wa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi''amesema Clouds Malunde 


Mkurugenzi wa CM Entertainment Clouds Charles Malunde ametumia nafasi hiyo kuiomba jamii hasa ya Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, Mwaka huu 2022 ili kuisaidia serikali katika kuweka mipango ya pajeti yenye kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.


Malunde amesema  baadhi ya wasanii wamesharekodi nyimbo za kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa lengo la kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.


''Tayari wasanii wamesharekodi nyimbo zipo za kuhamasisha sensa na tunamuunga mkono mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan watanzania wote tunapaswa kuhesabiwa kwa maana ya kwamba tuhesabiwe tupate kujulikana tupo idadi ya watu wangapi hatuna sababu ya watu kujificha ndani''.


''Sisi wasanii wa Mkoa wa Shinyanga tuko tayari kuhesabiwa kama kuna mtu yuko ndani siku hiyo tunaomba atolewe  watu wenye familia watakao kutwa ndani watoe ushirikiano ili tupate kujulikana kwamba tupo idadi ya watanzania wangapi lakini pia tunaishukuru serikali kwa sababu suala la sensa imeliweka kipaumbele sana kila sehemu tunasikia sensa''. amesema Malunde


Kwa upande wao baadhi ya wasanii wanaoshiriki tamasha hilo la kuhamasisha sensa ya watu na makazi akiwemo Mwenyekiti wa umoja wa wasanii Mkoa wa Shinyanga Daniesa Malula wamesema wanatumia vipaji vyao kuhakikisha wanafikisha ujumbe kwa wananchi ili kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Mwaka huu 2022.


Tamasha la kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi Mkoa wa Shinyanga limeanza leo ambapo litahitimishwa kesho Jumapili Agosti 21,2022 na kwamba baadhi ya wasanii wanaoshiriki ni kutoka makundi tofauti wakiwemo wasanii wa Bongo fleva, Hip Hop na wasanii wa nyimbo za asili pamoja na wasanii wanaofanya maigizo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post