Wakazi Shinyanga walia njaa,ni baada ya ardhi yao kupokonywa na Mamlaka ya Maji Shuwasa

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Baadhi ya wananchi wakiwemo wakazi wa kata ya Chibe na Old Shinyanga wameiomba serikali kupitia waziri wa maji Jumaa Aweso kushughulikia mgogoro wa Ardhi ambao umesababishwa na mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (SHUWASA) Manispaa ya Shinyanga.


Wakizungumza na vyombo vya habari wakazi hao wamesema kuwa mamlaka hiyo imewaondoa kwa nguvu bila kufuata utaratibu kwa  kutumia wafungwa na silaha kama Panga na kuwatishia silaha za moto ili waweze kuhama kwenye mashamba yao ambayo wamekuwa wakiyamiliki kwa muda mrefu ambayo yanasadikika yapo karibu na bwawa la Ning'wa linalopita kwenye vijiji mbalimbali ikiwemo kijiji cha Pandagichiza.


 Wananchi hao wamesema kuwa ni bora kama hawatakiwi kuwepo kwenye mashamba yao serikali ingetumia utaratibu wakuwapatia mashamba sehemu nyingine ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi kwani maisha yao yanategemea mashamba hayo.


Aidha katika hatua nyingine wananchi hao wamesema kuwa kama hali hiyo itaendelea kuwepo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani na kugharimu maisha ya watu pasipo na ulazima huo.


Donard Mbinzi mkazi wa kijiji cha Pandagichiza ni mmoja wa wahanga ambaye ameeleza huku akiiomba serikali kushughulikia, "Mimi ni mwenyeji wa hapa nimekulia hapa ila nasikitika kufyekewa shamba langu la mapapai heka moja mihogo ikang'olewa na SHUWASA wakakata na miti yangu wanasema kuwa ni eneo lao nimefika kwenye uongozi mpaka sasa wenyewe waliniahidi watakuja siku fulai lakini hawajafika ombi langu naiomba serikali inisaidie maana kupitia mapapai yangu na mihogo nilikuwa nasomeshea watoto wangu na kula sasa hivi wamekata naomba serikali inifikilie", amesema Donard Mbinzi


Amos Shija Gwalugwa naye ameeleza "haya Mimi nashangaa sasa kama ni serikali wao wanalitaka hili eneo kwanza nilasiku nyingi siyo la leo sisi humu yani tumezaliwa wajukuu mpaka tumekulia humu humu sasa imekuja kutokea fujo ambayo hatuijui sasa tunataka na sisi tupewe fidia''.


Mganga Lugandu naye amesema, " Nasikitika yakwamba mimi nataka kunyang'anywa maeneo yangu  heka 19 wakati wakutengenezwa hili bwawa limetengenezwa Mwaka 71 wakapima Mwaka 72 wakaweka majaribio kwanza Mwaka 73 ndiyo wakaanza kuzima wakamalizia Mwaka 74 kutoka Mwaka huo tulikuwa tunalitumia kama kawaida kwa nini sasa imefika kwa sasa tunaambiwa tuhame sasa tunaiomba serikali kama hili bwawa wamelipenda watulipe fidia ili tuende tukanunue maeneo mengine,".

Seni Punguja naye amesema hapo mwanzo waliambiwa wasilime ndani ya kilomita 60 na wakaamua kuacha kwa kuwa serikali imesema.

Bi. Pendo Edward Kasoga mkazi wa kata ya Chibe ambaye amesema eneo lake nipo karibu na bwawa hilo  Mwaka jana walikua hawa watu wa Magereza wakachimba miti na wakatukataza wakatuambia hakuna kulima katika haya maeneo haya wakasema tukiwaona tu mnalima hapa tunawapiga bunduki  na haya maeneo sisi tupo tunapopatia chakula na bado tunasomeshea watoto wetu basi tukaacha kulima Mama Samia tunaomba atusaidie sisi wanawake tunateseka tunaishi maisha ya shida walikuwa wapime mita 60 lakini wamepima mita Elfu moja kwahiyo sasahivi watoto hawaendi hata shule niko peke yangu tu yunifomu za shule nimekosa Mama Samia ninaomba utusaidie nimepiga magoti ututetee tunahangaika mimi ninaheka nane''.


Richard Msobi mkazi wa kijiji cha Pandakichiza naye ameeleza haya tunaomba serikali itusaidie hasa Mama Samia tunapoona sikia kwamba kilimo cha umwagiliaji kinaboreshwa basi na sisi sasa atuone kama ni wananchi wake ama wapiga kura wake ambao tunatakiwa tuwe na haki na sisi kama wengine tunakosikia na eneo hili ndiyo mahara petu pakulia tumeachwa enzi na enzi na mababu zetu na kama wanahitaji hao basi watufidishie kwa nini wengine tunasikia kwamba wanajengewa na nyumba, wanahamishwa vizuri tu wanakwenda kugawewa maeneo sasa ni kwanini sisi tu hata kama ni mwingine kweli ingekuwa imegeuka inageuka ikawe yeye anaeneo humu aje avamiwe kwa namna hii si atakubali tu kufa kwa ajili ya mali yako sasa tunamuomba sana Mamam Samia na viongozi wengine wote wa serikali waje watusaidie''.amesema Richard Msobi


Eneo ambalo limechukuliwa na bwawa la maji Ning'wa ni zaidi ya heka 200 lakini pia aneo ambalo linalalamikiwa na wananchi ambalo wamekuwa wakitumia kwa shughuli ya kilimo nalo ni zaidi ya heka 200.


Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (HUWASA) Manispaa ya Shinyanga  Eng. Yusuph Katopola amekiri kuwaondoa wananchi katika eneo hilo ili kulinda chanzo cha maji yanayoingia kwenye Bwawa la Ning'wa ambalo ni chanzo cha pili cha maji ukiondoa KASHWASA inayotoa maji ziwa victoria.


Mkurugenzi huyo wa SHUWASA Eng. Katopola amesema kuwa wao wanalinda chanzo hicho cha maji ili kisikauke kwani ni muhimu kwa mahitaji ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga.


Amesema  kuwa katika eneo hilo na Bwawa la Ning'wa yamekuwa yakifanyika matumizi mabaya ya chanzo cha maji kwa kutumia sumu wakati wa shughuli zao za kilimo na unyweshaji wa mifugo yao.


Eng. Katopola ameeleza kuwa SHUWASA imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi hao kuhusu umbali unaotakiwa kuachwa toka kwenye chanzo hicho cha maji ambacho ni mita 60 jambo ambalo wananchi hao hawataki kukubaliana nalo.


Aidha ametumia fursa hii kuwaomba wanakijiji hao kuhakikisha wanatii sheria na kulinda chanzo cha maji kwa ajili ya maisha ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga huku akiwakumbusha kuwa hata Waziri mkuu Kassim Majaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wamekuwa wakisisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji Nchini.


Bwawa la Ning'wa linahudumia taklimani asilimia 30 mpaka 40 ya eneo hote ambalo tunalihudumia sasa kutokana na changamoto iliyopo na kwamba hii Ning'wa kuna wenzetu wanajamii wa Shinyanga ambao wamekuwa wanatumia kwa shughuli mbalimbali hasa za kilimo lakini pia kunyweshea mifugo tumekuwa sisi tukijitahidi kulinda kile chanzo''.

Kama taasisi tulichukua jitihada za maksudi kabisa za kulinda kile chanzo mfano Miaka miwili nyuma kuzunguka Bwawa maeneo yote kulikuwa na shughuli nyingi sana za kilimo hasa mbogamboga ikiwemo nyanya, Bilinganya na mahiti walikuwa wanalima sana lakini kwa sasa hivi kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali za serikali tumeweza kupunguza hiyo hali ya shughuli za kilimu kuzunguka Bwawa''.


Kwa mfano kuna kipindi fulani tulienda na mkuu wa Wilaya tulikuta pale kuna makopo ya sumu kali yaani yale makopo yameandikwa kabisa kwamba dawa hii hairuhusiwi kutumia kwenye vyanzo vya maji tuliyaokota pale mengi sana kuonyesha kwamba wale wananchi waliokuwa wakitumia yale maji walikuwa wanatumia hayo madawa ili waweze kuvuna mazao mengi sasa tukiruhusu hiyo hali sisi mamlaka tunaingia kwenye changamoto nyingine kwanza tunaweza kutumia gharama kubwa kutibu yale maji lakini pili tunaweza kusababisha matatizo mengine ya kiafya kwa wananchi wengine kwahiyo kwa sababu hiyo kama taasisi tunajitahidi kwa nguvu zote kuhakikisha yale maji yakuwa salama kwa matumizi ya binadamu ndiyo lengu letu hakuna kitu kingine''. amesema Eng. Katopola 


Lile bwawa linazungukwa na kata tatu Chebe, Pandagichiza na Old Shinyanga kwahiyo hii elimu ilitolewa kwa wote lakini kama unavyotujua binadamu si wote wanaweza kuelimishwa wakakubali mfano tukifanya mkutano leo baada ya Mwezi mmoja au miwili wengine wanarudi wanafanya shughuli sasa sisi tulienda kwa lengo moja tu kwamba hatutaki palimwe tumeenda kuondoa vile ambavyo viko pale lakini wakati tunatekeleza yale majukumu wao ndiyo wakaanza  kuleta zile fujo na tulipozidiwa sisi tuliomba nguvu kutoka katika vyomvo vya usalama waje kutusaidia''. amesema Katopola 


Kisheria unatakiwa kutoka kwenye hicho kidaka maji uache mita 60 lakini bado niwaombe tena wananchi wote na wakazi wote wa Manispaa ya Shinyanga pamoja na maeneo jirani huduma ya maji ni huduma ambayo sisi wote tunaitaka  sana kwahiyo lazima tuwe tunafuatulia maelekezo ya viongozi wetu mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza mara kadhaa wote tulinde vyanzo vya maji waziri mkuu  Kassim Majaliwa alimwelekeza waziri wa maji lakini pia waziri wa maji yeye mwenyewe mheshimiwa Jumaa Aweso mara kadhaa ametoa maelekezo kwetu sisi wakuu wa taasisi tutunze vyanzo vya maji na amesisitiza tushirikiana na jamii mimi niwaombe tu wananachi wote tusaidiane kulinda hiki chanzo cha maji kwa manufaa ya wakazi wote wa Manispaa ya Shinyanga pamoja na maeneo jirani''. amesema Eng. Yusuph Katopola

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post