Vyuo vya nje vyatia fora maonyesho vyuo vikuu Dar

    Saurabh Chaudhary kutoka Chuo Kikuu cha GNA cha India akiwafafanulia wanafunzi kuhusu kozi zinazotolewa na chuo hicho kwenye banda la Global Education Link (GEL), wakati wa maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Wawakilishi wa vyuo vikuu vya nje ya nchi vinavyoshiriki maonyesho ya vyuo vikuu nje ya nchi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa Global Education Link ambao ndio wenyeji wao

 

*Baadhi vyapunguza ada kwa watanzania hadi asilimia 50

*Study in UK yaja na vyuo zaidi ya 154 kwenye banda la GEL

Ma

Na Mwandishi Wetu

VYUO Vikuu vya nje ya nchi vinavyoshiriki maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam vimekuwa kivutio kwa watu wengi.

Vyuo hivyo ambavyo viko kwenye mabanda ya Global Education Link (GEL), ni pamoja na MM, Sharda, CT, Geomedi, GELISM, Lovely Professional University, LPU, PDEU.

Vyuo vingine vya nje vinavyovyoshiriki maonyesho hayo yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ni vya kutoka nchi za India, Iran Cyprus, Uturuki, Georgia, Canada, Australia, Urusi, Dubai, Poland, Australia, Mauritius, Marekani na Uingereza.

Miongoni mwa vyuo hivyo kikiwemo cha CT cha India kilitangaza neema fani za tiba kwa kuwashauri wanafunzi watanzania kuchangamkia kozi za tiba zisizo za udaktari ambazo zinatolewa kwa gharama nafuu kwenye chuo hicho.

Chuo hicho kimetangaza punguzo la asilimia 50 kwa wanafunzi watanzania watakaodahiliwa kwenda kusoma kwenye chuo hicho ikiwa ni motisha ya kwa wengine kujiunga na fani hizo.

Neema hiyo ilitangazwa na Naibu Mkurugenzi wa chuo hicho, Gaurav Sharma, kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo vyuo vikuu 10 kutoka nje ya nchi vinashiriki kupitia mwamvuli wa Global Education Link (GEL).

Miongoni mwa vyuo vikuu hivyo ambavyo vimekuja nchini kwa mwamvuli wa Wakala wa Elimu Nje ya Nchi, Global Education Link (GEL) ni MM, Sharda, CT, Geomedi, GELISM, Lovely Professional University, LPU, PDEU.

 

 

Alisema wanafunzi wengi wa Tanzania wamekuwa wakichangamkia mafunzo hayo kutokana na kuwa na soko kubwa kwenye nchi mbalimbali duniani na kwa sasa kuna wanafunzi 100 wa Tanzania wanaosoma kwenye chuo hicho.

Alitaja kozi hizo kuwa pamoja na ufamasia, taaluma ya usingizi, teknolojia ya maabara, mionzi, teknolojia ya chumba cha upasuaji, physiotherapy (mamacheza) na Shahada ya Afya ya jamii.

Alisema nchi nyingi duniani zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa usingizi, mionzi na wale wa teknolojia inayotumika kwenye vyumba vya upasuaji na chuo hicho kimekuwa kikitoa wataalamu wengi kutoka mataifa mbalimbali.

Alisema chuo cha CT pia kimekuwa kikitoa wataalamu wa fani za akili bandia (artificial intelligence) na teknolojia ya hali ya juu kwa watu wanaofanyiwa matibabu ya moyo.

Alisema pia kimekuwa kikizalisha wataalamu wa kuhudumia wagonjwa mahututi na namna ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kuchujwa au kubadilishwa damu (Dialysis).

Mkurugenzi wa GEL, Abdulmalik Mollel, alisema wanafunzi wanaokwenda kusoma kwenye vyuo vya nje wamekuwa wakichota ujuzi na kurejea kusaidia taifa lao kwenye maeneo mbalimbali.

Alisema zamani wazazi waliogopa kuruhusu watoto wao kwenda nje ya nchi kusoma wakidhani kwamba hawatarejea lakini wengi wamekuwa wakichukua ujuzi na kuja kuutumia hapa nyumbani.

“Wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu wanapaswa kutembelea mabanda ya Global Education Link kwenye maonyesho ya Mnazi Mmoja kwasababu kuna uwakilishi wa vyuo 10 kutoka nje ambao watawaeleza kuhusu kozi wanazotoa na wataalamu wetu watawapa taarifa ili wawe na chaguo sahihi,” alisema

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post