Naibu waziri Katambi ahamasisha sensa Shinyanga

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Paschal Patrobas Katambi amewaomba wakazi wa Jimbo hilo kushiriki kikamilifu  zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo ni muhimu kwa mstakabali wa maendeleo ya Nchi.


Ametoa kauli hiyo leo wakati akihamasisha zoezi la Sensa  ya watu na makazi kwa wananchi katika maaeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa  ni sehemu ya ziara yake katika jimbo lake.


Mbunge Paschal Patrobas Katambi pamoja na mambo mengine amewasisitiza wananchi wa Jimbo la Shinyanga mjini kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo huku akiwataka kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu Sensa ya watu na makazi.


Amesema hatua hiyo itaisaidia serikali katika mambo mbalimbali ikiwemo kutenga bajeti kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.


“Imepita Miaka mingi ambayo watu wameongezeka wapo wameongezeka kwa kuzaliwa, wapo walioongezeka kwa kuhamia, kuzaliwa, wapo waliopata ulemavu lakini wapo waliopungua kwa maana ya kupumzika kwa haki sasa ikitokea hivyo ili muweze kuweka mipango vizuri  jumuishi ya maendeleo ni lazima kujua idadi kuwa kuna watu wangapi''.


''Ili serikali iweze kupanga mipango endelevu kutenga bajeti kwa usahihi na ufasaha lazima ijue Shinyanga wako wangapi wanahitaji nini kwahiyo ni muhimu sana sisi zote kuweza kuhesabiwa''. Amesema Mbunge Katambi


Mbunge Paschal Patrobas Katambi wakati akihamasisha zoezi la Sensa ametoa nafasi mbalimbali kwa wananchi kuuliza maswali ambapo wameipongeza serikali na kumshukuru Mbunge huyo kwa kuweza kuwatembelea kuwapatia elimu hiyo.


Wananchi hao wamesema wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali  inayowaletea maendeleo katika  nyanja mbalimbali huku wakiahidi kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa asilimia Mia moja.


Aidha pia baadhi ya wananchi wameuliza juu ya changamoto ya kupanda kwa bei ya bidhaa ikiwemo chakula ambapo naibu waziri Katambi ambapo amesema kuwa  Serikali inaendelea kushughulikia kikamilifu changamoto ya kupanda kwa bei katika bidhaa mbalimbali na kwamba hali hiyo iliyochangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo janga la uviko 19 pamoja na vita baina ya Urusi na ukrein.


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Paschal Patrobas Katambi ameendelea na ziara yake ya kikazi ambapo mpaka sasa ametembelea maeneo mbalimbali akisikiliza kero na kutafuta ufumbuzi wa  changamoto zilizopo katika Jimbo lake.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post