Mwanahabari Doreen ajitosa uchaguzi CCM

N Mwandishi Wetu, Dodoma

Mwandishi wa Habari wa kituo cha Upendo Tv Mkoani Dodoma Bi Doreen Aloyce  amejitokeza katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ujumbe wa NEC Taifa.


Doreen Aloyce  amesema ameamua kuchukua fomu hiyo ya kuwania nafasi ya mjumbe wa NEC Taifa baada ya kujitathimini kuwa anaweza na ana uwezo huo wa kukitumikia chama cha Mapinduzi CCM katika nafasi hiyo ya kuwa mjumbe wa NEC Taifa.


"Nimeona ninatosha na nina uwezo mkubwa katika nafasi hii muhimu katika chama changu kwa kuweza kumsaidia Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katika utendaji wake wa majukumu katika Chama cha Mapinduzi CCM na kwakuwa Chama chetu kwa sasa ndicho kinaisimamia serikali, hivyo kwa uwezo wangu nina hakika nitafanya vizuri"amesema Doreen Aloyce


Aidha Mwandishi huyo amesema kuwa anaitumia haki yake ya kikatiba ya Chama chake kuwa huru kugombea nafasi yote aitakayo katika chama chake katika nafasi yoyote.

" Pia nikiangalia nimekuwa ndani ya chama changu kwa muda mrefu kuanzia ngazi ya chipukizi, umoja wa vijana hadi sasa ambapo nimejiona ninatosha kuwania nafasi hii ya ujumbe wa NEC Taifa."


Mchakato huu  wa uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi CCM ,ambao unafanyika kila baada ya miaka mitano kwa ajili ya kuchagua viongozi mbalimbali wa chama kuanzia ngazi ya mashina, matawi, wilaya,mkoa na jumuiya zake katika ngazi zote hadi Taifa unaendelea kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM hapa nchini.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post