WAZAZI ACHENI TABIA YA KUWALAZA WATOTO WENU NA WAGENI WANAO KUJUA MAJUMBANI MWENU WANAWATENDEA WATOTO UKATILI

 

Uzinduzi wa Kampeni ya "MLINDE MTOTO WA KIUME'' Pichani ni tisheti imebeba ujumbe huo pamoja na Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika 2022
Inspekta wa Polisi Tadei Tarimo ambaye pia ni Polisi Kata ya Ngarenaro,Mkurugenzi wa Taasisi ya Vuka Initiative wakiwa katika Picha ya pamoja na watendaji wa Taasisi hiyo katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika 15june2022 katika kata ya Ngarenaro Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Vuka Initiative bi Veronica Ignatus Akiwa ameshikilia bango lenye Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika Kata ya Ngarenaro.15juni 2022
Wa kwanza kushoto ni diwani wa kata ya Ngarenaro Isaya Doita Harry  ,akifuatiwa na mgeni rasmi wa Diwani wa Kata ya Moshono Miryam Kisawike,pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vuka Initiative Vero Ignatus wakikata keki ishara ya Uzinduzi wa Kampeni ya "MLINDE MTOTO WA KIUME''
Mkurugeni wa Taasisi ya Vuka Initiative akimlisha keki mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya MLINDE MTOTO WA KIUME''iliyofanyika 15juni2022 kwa ngazi ya kata ya Ngarenaro 
Mkurugenzi wa Vuka Initiative bi Vero Ignatus akiendelea na kugawa keki kwa meza kuu Mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya 'MLINDE MTOTO WA KIUME''iliyofanyika siku ya Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Ngazi ya Kata ya Ngarenaro
Baadhi ya Wanafunzi walishiriki katika siku ya mtoto wa Afrika Kata ya Ngarenaro iliyoambatana na uzinduzi wa Kampeni ya MLINDE MTOTO WA KIUME''ambayo ilifanywa na Taasisi ya VUKA INITIATIVE
Baadhi ya vijana kutoka Taasisi ya Vuka Initiative wakiwa wameshiriki maandamano kwaajili ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika ngazi ya kata Ngarenaro 15 Juni 2022
Baadhi ya Wanafunzi walishiriki katika siku ya mtoto wa Afrika Kata ya Ngarenaro iliyoambatana na uzinduzi wa Kampeni ya ''MLINDE MTOTO WA KIUME''ambayo ilifanywa na Taasisi ya VUKA INITIATIVE

WAZAZI ACHENI TABIA YA KUWALAZA WATOTO WENU NA WAGENI WANAO KUJUA MAJUMBANI MWENU WANAWATENDEA WATOTO UKATILI

 Na.Mwandishi wetu Arusha

Wazazi na walezi wameaswa kutokuwalaza  watoto wao na wageni wanapotembelea majumbani mwao kwani baadhi yao  wanawatendea watoto hao Ukatili bila wao kujua

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la  Vuka Initiative Bi.Veronica Ignatus  walipokuwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyoambatana na uzindua Kampeni ya "MLINDE MTOTO wa KIUME'' Kata ya Ngarenaro 15/6/2022 yenye Lengo la kuwakumbusha Wazazi umuhimu wa  kuwajengea watoto msingi imara kwani ndiyo Baba wajao

"Tusipowajengea msingi imara watoto wetu haswa wakiume tutakuja kuwa na familia za aina gani?tukiwaacha watoto wetu bila kuwalinda wakalawitiwa tutakuja kuwa na Viongozi wa aina gani jamani ?alihoji "

"Hakuna kuaminiana ni kheri uchukiwe na ndugu lakini uponye kizazi chako,hao mnaowaona wema na kuwakaribisha na kuwalaza na watoto wenu , wakati mwingine wamekuwa wakiwatishia watoto na wao kuingiza woga kusema vitendo vya kikatili wanavyotendewa"

Bi Veronica alisema kwamba asilimia kubwa ya watoto wanatendewa Ukatili na ndugu wa karibu waliopo majumbani mwao,mbapo kwa asilimia kubwa ni ndugu wa mume au mke au marafiki ambao familia hizo zimewaamini na kuwakaribisha

Amesema hali hiyo ya Ukatili  kwa watoto inakuja katika kipindi hiki ambacho wazazi na walezi wengi wanatajwa kutokuwa karibu na watoto wao, wengi wakijihusisha na kusaka maisha bora ili kukidhi mahitaji ya msingi ,huku wakikosa haki ya  haki ya kuwasikiliza.

"Mgeni Kama ameweza kijisafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine anakuja kutembelea nyumbani kwako, na unafahamu kuwa nyumba yako haina vyumba vya kutosha kumkimu kwanini usimtafutie nyumba ya wageni akapumzike huko hadi siku atakavyoona vyema atakavyoondoka?"

Akizungumza mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo yaliyofanyika kikata diwani wa kata ya Moshono Miryam Kisawike aliwataka Wazazi kuwa makini katika hatua za ukuaji wa mtoto kwani kufanya hivyo kutaepusha hatari nyingi ambazo zingempata mtoto.
 
''Watoto wetu ni tunu ambayo Mungu ametupa tuitunze,sasa mzazi unapokuwa bize umjali huyu mtoto unadahania ni nani atakusaidia kumlea? tuwe wakweli unaposikia mtoto ametendewa ukatili wa kulawitiwa au kubakwa kwakweli inaumiza sana sana,hebu jamii yote tuungane kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama ''alisema Miryam Kisawike

Kwa uande wake Inpekta Happy Adinani Mshana kutoka Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha, amewaonya Wazazi kuacha tabia ya kupoteza ushahidi wa kesi kwa kutetea uovu,kwa sababu ya kulinda hadhi ya familia,Sambamba na baadhi ya waalimu kuacha kutoa taarifa pale mmoja wao anapomfamyia mwanafunzi ukatili kuacha tabia hiyo Mara moja.

Sambamba na hayo aliwataka Wanafunzi kuacha tabia mbaya ya kuingiliana kinyume na maumbile kwani baadhi yao wamekuwa wakitunika kuwaingilia watoto wadogo wa shule za msingi jambo ambalo ni baya na linaharibu malengonyaonya kuja.akuwa baba Bora wa baadae.

"Hatufichani nyie Wanafunzi wa sekondari mnanielewa kwani baadhi yenu mmekuwaa na tabia mbaya ya kutumika kwa wadogo wenu wa shule ya msingi,Leo unafanya hicho kitendo hicho ni kibaya Leo na kesho unafanya kitendo hicho unaharibu malengo yako ya kuja kuwa baba Bora wa baadae"Alisema.
 
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ngarenaro Isaya Doita Harry aliwashukuru wageni wote walioshiriki katika maadhimisho hayo na kusema kuwa ukatili wanaofanyiwa watoto haukubaliki kamwe,hivyo jukumu kla kuwalinda watoto ni la kila mmoja kuhakikisha watoto wanakuwa salama
 
''Wazazi tunawaomba sana kutoa ushirrikiano pale ambapo mtoto amefanyiwa ukatili wakati mwingine hao wanaowatendea watoto wenu ukatili mnawafahamu ila mnawaficha hamtaki wajulikane mnawatunzia siri na kumaliza kesi hizo kimyakimya kifamilia,niwaambie ukweli mnawaumiza watoto wenu,tupeni ushirikiano ili watoto wabakie salama na kutuimiza ndoto zao za baadae''Alisema Doita
 
Aidha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka 16juni ila kwa kata ya Ngarenaro yalifanyika 15juni 2022 yakiwa yamebeba Kauli mbiu isemayo ''Tuimarishe Ulinzi wa Mtoto,Tokomeza Ukatili Dhidi yake''Jiandae kuhesabiwa 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post