Watafiti wa miamba waitwa Kolo

Mhifadhi Amoni Mgimwa kutoka Katika kituo cha kivutio cha miambani Kondoa Kolo

Na Queen Lema, Kondoa

Watafiti wa vyuo vikuu hapa nchini wametakiwa kufanya utafiti kwenye michoro ya miamba ya kolo kondoa Mkoani Dodoma ili  kuwezesha upatikanaji na ufumbuzi wa mambo mbalimbali ambayo yalichorwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.


Imeelezwa kwamba  mpaka sasa kuna mawe 1000 ambayo   bado yanatakiwa kufanyiwa utafiti  wa kwenye michoro ya miamba ya Kolo Kondoa Dodoma huku yaliyofanyiwa utafiti pekee ni mawe 480


Hayo yameelezwa na Amoni Mgimba ambaye ni mhifadhi  daraja la kwanza,kutoka katika kituo cha michoro ya miambani Kolo Kondoa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walitembelea  vivutio mbalimbali wiki iliyopita



Mgimwa alisema kuwa vivutio vya  michoro ya miamba ni moja ya vivutio ambavyo vimekuwa vikionesha mambo mbalimbali hasa ya kizazi cha kale 


Alisema kuwa kupitia michoro hiyo ya mapangoni fursa nyingi sana zimeweza kuibuliwa huku Jamii pamoja na taifa  ikipata faida 


"Tunaweza kuona faida ambayo vivuo hivo vimepata moja ni kutangaza Tanzania Duniani sasa utafiti ukiwa umekamilika Kwa mawe hayo 1000 tutafika mbali sana "aliongeza


Mhifadhi huyo alisema kuwa mpaka sasa mawe ambayo yamechorwa yapo Zaidi ya 480 natayari imefanyiwa tathimini na watafiti toka  ndani na nje ya nchi huku miamba mingine 1000 ikiwa bado inaitaji utafiti 


Katika hatua nyingine alisema kuwa michoro hiyo ya miambani inawakilisha urithi unaoishi(the Living Heritage)hivyo hata watanzania nao wanatakiwa kutembelea vivutio hivyo 


"Sisi tunaweza kusema kuwa hapa tuna Utalii kama Utalii lakini pia Utalii huu imebeba maana halisi ya utamadani hasa wa watanzania na ndio maana waliochora waliochora ili kuifadhi Mila na desturi"aliongeza


Aliwataka hata watanzania kuhakikisha kuwa wanatembelea na kutangaza vivutio  na kuwa sehemu ya Utalii na kuachana na tabia ya kuona wanaostaili Utalii ni watu wa nje ya nchi pekee.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post