Vijana wa UVCCM zaidi ya 1,000 ndani ya Hifadhi ya NgorongoroNa Mwandishi Wetu, Ngorongoro


Ujumbe wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) zaidi ya 1,000 wakiongozwa na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Kenani Kihongosi umewasili katika Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kufanya utalii wa vivutio mbalimbali vilivyopo ndani Hifadhi hiyo.


Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa ndugu Kenan Kihongosi ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye fimalu ya The Royal Tour ambayo imeonyesha vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Nchi yetu. 


“Vijana hawa zaidi ya 1,000 wamekodisha magari ya utalii 140 na wameamua kujigharamia kuja hapa Ngorongoro kuona vivutio tulivyonavyo ili kusaidia kutoa hamasa na chachu  kwa watanzania wengine wajue kuwa Utalii unaanza na sisi wenyewe ili tuwe mabalozi wa kuhamasisha wageni wengine wa nje ya Nchi kukutembelea” alifafanua Kihongozi


Ameongeza kuwa uwepo wao katika maeneo ya Wilaya za Karatu na Ngorongoro umesaidia kuongeza mzunguko kwa wajasiriamali hasa Hoteli, Magari ya utalii, biashara za vyakula kwa mama lishe hivyo kusaidia uimarishaji uchumi wa wananchi katika kusukuma agenda ya maendeleo na kuwaambia watu kuwa utalii ni fursa na utalii ni ajira. 


Akipokea Ujumbe huo Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Raymond Mwangala amewashukuru UVCCM kwa kuunga mkono jitihada za Rais na Serikali yake kuhamasisha utalii wa ndani kwa vitendo kwa kuamua kuchangishana kwa kwa idadi kubwa kutembelea vivutio vya Ngorongoro kwa pamoja. 


Ameeleza kuwa Vivutio vya Ngorongoro ni vya kipekee na baada ya uzinduzi wa Filamu ya Royal tour anaamini wageni wataongezeka na kuongeza mapato ya Serikali ambayo yataongeza uchumi wa Nchi na kusaidia Serikali katika ujenzi na uimarishaji wa huduma zingine za kijamii kwa wananchi wake.


Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi Elibariki Bajuta anayesimamia huduma za Ulinzi NCAA ameuhakikishia ujumbe huo kuwa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni Salama, tulivu lenye vivutio vya Kila aina na Serikali kupitia NCAA inaendelea na juhudi za Uhifadhi na uboreshaji wa miundimbinu ya Utalii ili wageni wanaotembelea Hifadhi hiyo kupata huduma bora muda wote.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post