Passsf wajipanga kuwekeza Zanzibar

Meneja wa Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF,James Mlowe,Waziri wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Simai Mohamed Saidi,wakati wa ufungaji wa maonyesho ya biashara Tanga 06 June 2022.
Meneja wa Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF,James Mlowe akiwa na wafanyakazi wenzake wakati wa ufungaji wa maonyesho ya biashara,Tanga.

Na Mwandishi Wetu,Tanga


Mfuko wa Huduma za Jamii PSSSF imesema tayari imeshaanza kutekeleza miradi ya uwekezaji Zanzibar ambao utakua ni uwekezaji katika kisiwa hicho ambao utakua na tija kwa kuongeza uchumi.

Katika kuhakikisha wanaendeleza agenda ya utalii kitaifa PSSSF imeanza ujenzi wa miradi ya maendeleo katika kisiwa cha zanzibar.

Akizungumza mbele ya Waziri wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Simai Mohamed Said,Meneja wa Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF,James Mlowe kwenye maonyesho ya biashara Tanga,amesema wameamu kufanya uwekezaji ambao utahamasisha utalii kwa kiasi kikubwa katika visiwa vya Zanzibar.

Uwekezaji huo ni wakujenga kituo kikubwa cha mikutano Zanzibar pamoja na kujenga vituo vya kisasa za dalada,pamoja na stand ya mabasi

"Katika mambo ambayo PSSSF inayafanya ni uwekezaji,tuna miradi ambayo tumeanza kutekeleza Zanzibar,kwanza kuna(International Conference Center) ukumbi wa kimataifa wa kisasa zaidi,kuna ujenzi wa miradi ya vituo vya daladala za kisasa na stand za kisasa,ambayo kwa sasa tupo kwenye visibility study"alisema Mlowe

Mlowe amesema kuwa kwa sasa PSSSF inafanya shughuli mbalimbali za kijamii na kwa sasa Taifa agenda kuu ni Utalii,hivyo ndio sababu kuu ya kufanya uwekezaji.

Mlowe ameeleza kuwa PSSSF itaendeleza utamaduni wa huduma bora kwa mteja na iliyotukuka kwa wanachama kuwa ni haki ya kila mmoja.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post