Lise Academy washirikiana na Halmashauri ya Kibaha kupanda miti

Wageni mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa shule za awali za Lise, Yusuph Chanyika wakichukua miti kwaajili ya kuiboresha ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mazingira duniani 6 Juni 
Wananchi wa Niko Timiza wakichukua miti
Mkurugenzi wa mazingira Wilaya ya Kibaha Ally Khatibu akishiriki zoezi la kupanda miti
Mkurugenzi mtendaji wa shule za Lise Academy Mainda Chanyika akiwa kashikilia mti tayari kwa kuuotesha
Mkurugenzi wa shule ya Lise  Mainda Chanyika akiotesha mti
Mkurugenzi Mkuu wa Lise Academy Yusuf Chanyika akikagua mti aliouotesha
Mainda Chanyika Mkurugenzi mtendaji wa Lise Academy akizungumza na waandishi wa habari
Hemed Athumani  mmoja wa wadau na diwani katika moja ya kata za Wilaya ya Kibaha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi la kupanda miti
Wanafunzi wa shule ya awali ya Lise Academy wakishuhudia zoezi la upandaji miti

 

Na Mwandishi Wetu, Pwani

Uongozi wa shule za awali za Lise Academy zilizoko Biko Tumiza Kibaha, umeungana na Serikali ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kupanda miti ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ukame na kutunza mazingira.

Akizungumza katika zoezi la uoteshaji wa miti ikiwa ni maadhimisho ya siku ya upandaji miti duniani, Mkurugenzi Mkuu wa shule za awali za Lise Yusuph Chanyika, amesema wameshirikisha watoto katika zoezi hilo ili kuwajengea msingi wa kupenda kutunza mazingira na kujua umuhimu wake.

Amesema kwa watu wenye umri unaolingana na kama wake kama hawajui umuhimu wa mazingira hata ukitumia nguvu na mbinu gani ni vigumu kuelewa lakini ni rahisi kwa watoto kujua umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa kuwa wanaendelea kukua.


Chanyika amesema " Mtoto mdogo ukimpatia elimu sahihi ni rahisi kukuelewa na kutenda na akielewa baadae ataelimisha na kizazi chake,"amesema.


Amesema ofisi yake imenunua miti 300 na tayari wameshapanda miti120 kwenye zahanati iliyoko karibu na shule za awali za Lise na kwamba zoezi hilo litaendelea  kwenye taasisi za Serikali ambazo zina uhaba wa miti.

Mkurugenzi mtendaji wa Lise Academy,  Mainda Chanyika amesema wametoa maelekezo kwa wanafunzi kufika shuleni na lita moja ya maji kila siku kwaajili ya kumwagilia miti hiyo na kwamba wanaimani miti hiyo itakuwa bila shida yoyote.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa mazingira wilaya ya Kibaha Ally Khatibu ameushukuru uongozi wa shule za awali za Lise kwa kazi nzuri inayofanya na kwamba kabla ya kuanza kupanda miti hiyo ilitolewa elimu ya utunzaji wa mazingira na namna bora ya upandaji wa miti.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post