Watumiaji wa gesi watakuwa kuhakiki uzito kabla ya kuitumia

Picha ya washiriki  wa mkutano ulioandaliwa na taifa gesi

 Na Mwandishi Wetu, Arusha

Wafanyabiashara wa gesi wametakiwa kutumia mizani kupima uzito wa mitungi ya gesi ili kujua kama imejaa au iko pungufu  na kuachana na tabia ya kuuuza gesi bila kupima 


Hata hivyo imeelezwa kwa sasa bado wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao wanauza mitungi ya gesi bila kupima jambo ambalo ni  kinyume na sheria kwani uzito unatakiwa kuonekana kabla ya mtumiaji kufikisha nyumbani na kuanza matumizi


Hayo yameelezwa na mhandisi.     Lorivii Long'idu Kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(Ewura)   Wakati akiongea na wauzaji wa gesi za majumbani mapema leo Jijini hapa kwenye semina ambayo imeandaliwa na kampuni ya Taifa gesi.


Mhandisi Lorivii alisema kuwa wanawajibu wa kumuuzia mtuamiaji kilo ambazo zimeoneshwa kwenye mtungi


"Mwananchi unatakiwa kuhakikisha kuwa umeona muuzaji akiwa amepima na umejiridhisha kabisa kuwa ni kiwango hicho lakini Kama ni pungufu basi pia utaona"


Aliongeza kuwa wafanyabiashara wa uuzaji wa mitungi hiyo ya gesi  wakifuata sheria basi changamoto hizo za ujazo hafifu zitaisha kabisa.


Aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanakuwa waaminifu na kuachana na tabia ya kupunguza gesi kwani endapo watakamatwa sheria itawafikisha mahakamani.


"Tulifanya msako Moshi na tumeshawafikisha mahakamani wafanyabiashara wawili niwaombe tu ninyi wafanyabiashara wanaofanya hivyo waache kwani ni hatari sana ndani ya jamii"aliongeza.


Naye Bw Joseph Nzumbi ambaye ni meneja mauzo  kutoka Taifa Gas alisema kuwa bado kwa mikoa ya Kaskazini kuna changamoto ya ujazaji wa mitungi ambayo imejazwa mitaani jambo ambalo sasa watu


Aliwataka watumiaji wa gesi na wenyewe  kabla hawajatumia kuhakikisha zimepimwa lakini ziwe na ubora sanjari na uzito ulioandikwa  kwenye mitungi 



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post